Habari za Punde

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mwaboya Akanusha Habari Zilizoenea Katika Mitandao ya Jamii Kuhusiana na Kupanda Kwa Nauli za Daladala.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mwaboya akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kukanusha habari zilizoeneo katika mitandao ya Kijamii kuhusiana na kupandishwa kwa nauli za daladala na kusema taarifa hiyo sio ya ukweli  Wizara yake haijatoa bei mpya za nauli za daladala, Na kuwataka wananchi kulipa nauli hiyo ya zamani na kupuuza taarifa hizo sio za ukweli.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar alipokuwa na mazungumzo na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vilioko zanzibar kuhusiana na kukanusha habari za ufumi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kupendisha bei ya nauli za daladala habari hizo si za kweli na nauli inabaki kuwa ileile na kuwataka wananchi walipie nauli hiyo ya zamani mpata itakapotolewa taarifa rasmin na Taasisi husika na Usafirishaji Zanzibar. mkutano huo umefanyika katika ukumbi mdogo wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Waziri wa Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Dkt. Sira kuhusiana na uvumi wa kupanda kwa nauli ya daladala Zanzibar. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.