Habari za Punde

Jeshi la Polisi lawashikiliwa Watuhumia Kwa Kujishughulia na Uuzaji Pombe Haramu.

JESHI la Polisi la Mkoa wa Kaskazini Unguja linamshikilia Suzana Fabian Albet mwenye umri wa miaka (60) mkaazi wa Kitope Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa kujihusisa na dawa za kulevya.
Likiwa kwenye operesheni za kuwatafuta waingizaji, wasambazaji na watumiaji wadawa hizo, katika mkoa huo walimtia mbaroni bibi huyo akiwa na pombe ya kienyeji (gongo).
Kamanda wa polisi wa Mkoa Kaskazini Unguja Kamishina Msaidizi wa Polisi, HajiAbdalla Haji akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, alieleza kuwa bibi huyoalikamatwa na pombe ya kienyeji ikiwa kwenye chupa saba zenye ujazo wa lita moja na nusu kila chupa.
Suzana alikamatwa Septemba 20 mwaka huu majira ya saa 2:00 asubuhi huko KitopeMuembe majogoo wilaya ya Kaskazini ‘B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mbali ya Suzana pia jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata Vuai Schowel Kimada (55) mkaazi wa kijiji hicho hicho alipatikana na ulevi kama huo pamoja na mitambo yake, Septemba 16 mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku katika kijiji hicho.
Bwana Vuai alipatikana akiwa na dumu mbili na nusu za ulevi pamoja na mtambo wake wa kupikia gongo.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.