Habari za Punde

Kamati za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Kwa Ubia na Sekta Binafsi.










Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, 
Bajeti na Kamati ya Uwekezaji na Mitaji, wameishauri 
Serikali kutekeleza kwa vitendo miradi mikubwa na yenye tija 
kwa Umma kwa kutumia njia ya Ubia kati ya Umma na Sekta 
binafsi ili kuchochea haraka maendeleo ya nchi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya 
Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa wabunge 
wameridhishwa na na hatua zinazochukuliwa na Serikali 
katika kuhakikisha kuwa mpango wa ubia kati ya Serikali na 
sekta binafsi unafanikiwa na unachochea maendeleo ya 
wananchi.

“Kama wabunge tungependa kuona mpango unaingizwa 
katika mipango ya Serikali ili kuharakisha miradi ya 
maendeleo na pia tunapongeza hatua zilizochukuliwa na 
Serikali ikiwemo kumteua Kamishna anayeshughulikia 
miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ile ya umma, “ 
Alisisitiza Mboya

Alibainisha kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa 
inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wote 
watakaojitokeza kushirikiana na Serikali katika kutekeleza 
miradi ya maendeleo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi 
Mhe. Endrew Chenge amesema kuwa nchi nyingi Duniani 
zimefanikiwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia 
utaratibu huo ambapo jambo la muhimu ni kufanywa kwa 
maandalizi ya kina na kuwepo kwa utashi kutasaidia 
kufanikiwa kwa miradi husika .

Aliongeza kuwa mwaka huu Serikali imeleta Bungeni 
Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya PPP utakaojadiliwa na 
wabunge katika Bunge linaloanza Septemba 4 mwaka huu, 
pamoja na mambno mengine Muswada huo unapendekeza 
kuanzishwa kwa Kituo cha PPP chini ya Wizara ya Fedha na 
Mipango, ambacho kitakuwa na jukumu la kuishauri Serikali 
kuhusu masuala yanayo husu miradi mbalimbali 
itakayowasilishwa kwa mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya 
Umma na Sekta Binafsi

Akizungumza katika Semina hiyo, Kamishna  wa Ubia kati ya 
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na 
Mipango, Dkt. John Mboya amesema kuwa Dhamira ya 
Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi 
katika kutekeleza miradi ya ubia na Sekta binafsi ili kuleta 
mageuzi katika maisha ya wananchi.

“Lengo la kuwa na miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta 
binafsi ni kutekelezaIilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), 
kutekeleza mpango wa maendeleo na hatimaye kutoa 
huduma bora kwa wananchi,” Alisisitiza Mboya

Akifafanua Mboya amesema kuwa moja ya hatua za 
maboresho zilizochukuliwa na Serikali ni kuhamisha Kituo 
cha kusimamia miradi ya ubia katika ya Umma na Sekta 
binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuja Wizara ya Fedha.

Akizungumzia majukumu ya chombo cha kusimamia 
utekelezaji wa miradi hiyo Dkt. Mboya  amesema kuwa 
chombo hicho kimepewa jukumu la kufanya uchambuzi wa 
kina kuhusu miradi yenye sifa na kusimamia mchakato wa 
uteklezaji wa mpango huo kwa kufuata ngazi zote zilizopo 
hadi utekelezaji wa mradi husika.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha mpango huo Serikali 
inasisistiza uwazi, uwajibikaji na utayari hali itakayo 
sababisha  kufikiwa kwa malengo ya miradi ya ubia kati ya 
sekta hizo mbili ambapo alitaja baadhi ya miradi 
itakayotekelezwa ambayo upembuzi yakinifu umekamilika 
kuwa ni ile ya ujenzi wa Viwanda vya dawa, usambazaji wa 
gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara , Lindi 
na ule wa uendeshaji wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar 
es Salaam ambao umeanza na uko katika hatua mbalimbali 
za uendelezwaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya 
Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa tayari 
Bohari hiyo imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa 
ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na 
malighafi zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo pamba na 
kufikia machi mwakani zabuni ya mradi huo itatangazwa ili 
kuwapata wabia.

Katika kutekeleza mradi huo kiwanda cha kuzalisha maji ya 
dripu yanayotumika kwa wagonjwa mahosipitalini pia 
kitajengwa ambapo kwa sasa maji hayo yanaagizwa kutoka 
nchini Uganda na kwamba hatua hiyo itapunguza gharama 
za Serikali za kuagiza dawa na vifaa hivyo kutoka nje ya nchi 
ambapo zaidi ya shilingi trilioni 1.8  hutumika kuagiza 
bidhaa hizo kila mwaka.

Kwa upande wake. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la 
Maendeleo ya Petroli (TPDC) Mhandisi Kapuulya  Musomba 
amesema kuwa mradi wa kusambaza gesi majumbani katika 
Jiji la Dar es Salaam, Mtwara na Lindi unaotarajiwa 
kuhgaribu zaidi ya shilingi bilioni 300, utaleta mageuzi kwa 
wananchi wa mikoa hiyo ambapo wananchi zaidi ya 120,000 
katika Jiji la Dar es Salaam watafikiwa.

Aliongeza  kuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara wananchi 
zaidi ya 5,000 wataunganishiwa gesi majumbani mwao huku 
viwanda zaidi 30 katika maeneo ya mradi vitaunganishiwa 
huduma hiyo pamoja na vituo vya kujaza gesi kwenye magari 
yanayotumia nishati hiyo.

Semina kwa wabunge wa Kamati za Bajeti, Miundombinu na 
ile ya Uwekezaji Mitaji imefanyika Jijini Dodoma 
ikiwashirikisha wajumbe wa Kamati hizo ili kuwajengea 
uwezo wa namna dhana hiyo inavyoweza kuleta maendeleo 
hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.