Habari za Punde

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali Azindua Msimu Mpya wa Uchumaji wa Karafuu Kisiwani Pemba.

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi , Amina Salum Ali, akihutubia Wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi wa uchumaji wa Karafuu kwa msimu huu 2018,Kisiwani Pemba Uzinduzi huo umefanyika katika Kijiji cha Ngomeni.   
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba, walihudhuria katika Uzinduzi wa Msimu mpya wa uchumaji wa Karafuu huko katika Kijiji cha
Ngomeni Pemba.
Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Msimu mpya wa uchumaji wa karafuu uliofanyika katika Kijiji cha Ngomeni Kisiwani Pemba.

Wananchi mbali mbali wa Kisiwa cha Pemba wakiwa katika Sherehe za uzinduzi wa msimu mpya wa uchumaji wa Karafuu  iliofanyika katika kijiji cha Ngomeni Chake Chake Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.