Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Malindi Zanzibar Wakijiandaa na Michuano ya Bonaza la Ujamaa na Maandalizi ya Ligi Kuu ya Zanzibar Msimu Ujao 2018/2019.

Wachezaji wa Timu ya Malindi Zanzibar wakiwa katika uwanja wao wa Mnazi Mmoja wakimsikiliza Kocha wao mchezaji wa zamani wa Timu hiyo Waziri Seif baada ya kumaliza mazoezi yao wakati wa asubuhi wakijiandaa na Michuano ya Tamasha la Bonaza la Timu ya Ujamaa na Ligi Kuu ya Zanzibar inayotarajiwa kuaza kutimu vumbi hivi karibuni Visiwani Zanzibar.
 Timu ya Malindi imepanda daraji msimu huu na baada ya kusota kwa muda mrefu daraja la kwanza  na hatimai kufanikiwa kurudi katika Ligi Kuu ya Zanzibar kwa Msimu wa 2018/2019.
Kikosi cha Timu ya Malindi kinaundwa na sura mpya nyingi baada ya kufanya usajili wa kusajili wachezaji kutoka Timu ya Taifa ya Jangombe ilioshuka daraja msimu wa ligi Kuu ya Zanzibar 2017/2018. 
Kikosi hicho kikinolewa na Kocha wake Mkuu Saleh Machupa kwa ajili ya kujianda na Ligi Kuu ya Zanzibar kwa msimu wa 2018/2019.

Mwenyekiti wa Mpya wa Timu ya Malindi Zanzibar Ndg. Mohammed Abdallah Al Jabir, akifuatilia mazoezi hayo kuhakikisha Timu yake inafanya vizuri michuano ya Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu wa 2018/2019. Na kuhakikisha timu hiyo inakuwa imara katika timu zote zinazoshiriki ligi hiyo, na kuwataka wanachama wa Malindi kujitokea kuishangilia timu yao kwa hali na mali ili kuweza kurudisha heshima ya enzi zake katika miaka ya nyuma.kushoto Koccha Mkuu wa Timu hiyo Saleh Machupa wakiwa katika Uwanja wao wa Mnazi Mmoja Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.