Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo.

Na Mwashungi Tahir  na Fatma Makame            Maelezo  20-
9-2018.

Serikali inaendelea kuendeleza jitihada za kuondoa  biashara 
haramu ya ukahaba na mapenzi ya jinsia moja kwa Mkoa wa 
Mjini Magharibi umefanikiwa kuwakamata wahusika 35 na 
hatua za kisheria zinaendelea ikiwemo kupelekwa 
Mahkamani.

Hayo ameyasema leo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za 
Mikoa ,Serikali Za Mitaa na Idara Maalum Za SMZ Shamata 
Shaame Khamis  huko kwenye ukumbi wa Baraza la 
Wawakilishi  wakati alipokuwa akijibu suala la Mheshimiwa 
Jaku Hashim Ayoub wa Jimbo la Paje aliyetaka kujua Je ni 
watu wangapi waliokamatwa na kufikishwa Mahakamani.

Alisema Malengo ya Operesheni hiyo imefanikiwa kwa kiasi 
kukubwa ambapo imeweza kudhibitiwa kwa muda wa 
kuanza na kumaliza burudani za muziki katika kumbi za 
starehe, aidha imeweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa ya 
matumizi ya shisha , udhalilishaji wa kijinsia na kusimamia 
utaratibu wauzaji na matumizi ya video kwa muda wa saa za 
kazi.

Pia Mkoa bado unaendelea na zoezi la kufanya operesheni ya 
kushtukiza katika kumbi za starehe , vilabu vya pombe na 
madanguro kwa lengo la kudhibiti kadhia hizo.

Aidha alisema zoezi linaendelea kutokana na malengo 
tulojiwekea pamoja na kupata taratibu za sheria ikiwemo 
jeshi la polisi kutoa elimu kwa jamii juu ya kutii sheria bila 
ya kushirikishwa kutoa barua kwa maeneo yanayohusika 
kwa biashara ya ukahaba ikiwemo Entebbe , Nyuki , 
Mwanyanya , Gofu na Mafunzo na kufungia madanguro 
maeneo ya Miembeni pamoja na kuimarisha doria ya 
kudhibiti madada na makaka poa.

Akiongeza suala la nyongeza Mh Jaku aliuliza kwa nini 
harakati hizi za kudhibiti mambo haya mbona hazijagusa 
watu wanaofanya vitendo vya jinsia moja.

Nae Naibu Waziri alimjibu kuwa wao wameamua kufanya 
kwa wote wanaohusika na mambo ya ukahaba bila ya 
ubaguzi wowote.

“Sisi tunawakamata wale wote wanaojihusisha na mambo ya 
ukahaba na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia bila 
kubagua watu wa aina gani sheria inafata mkondo wake”. 
Alisema Naibu Waziri huyo.

Nae Naibu Waziri wa Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali 
Mmanga Mjengo Mjawiri akilijibu suala la Mh Ali Suleiman 
Ali wa Jimbo la kijitoupele aliyetaka kujua Je Wizara ina 
mpango gani wa kulinda usalama wa wanafunzi  wa Skuli za 
binafsi ambao wanajazwa sana katika magari.

Akijibu suala hilo Naibu huyo huko kwenye ukumbi wa 
Baraza la Wawakilishi alisema wizara bado inatambua kuwa 
baadhi ya magari ya skuli binafsi yanayopakia wanafunzi 
yanajaza kupita kiasi jambo ambalo linaweza kuhatarisha 
usalama wa wanafunzi hao .

Alisema Wizara imekua ikilikemea suala hili katika mikutano 
mbali mbali iliyofanyika na Skuli za binafsi au viongozi wa 
umoja wa skuli hizo pia imewasilisha suala hili kwa kamanda 
wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na kutaka askari wa 
usalama wa barabarani wawachukulie hatua za kisheria weye 
magari wote watakaobainika wanakiuka taratibu za usalama 
barabarani.

Mwisho.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.