Habari za Punde

Kwesi Nyantakyi: FIFA Yamuongezea Muda wa Marufuku Rais wa Soko Ghana Kwesi Nyantakyi

Rais wa Chama cha Mpira Nchini Ghana Kwesi Nyantakyi, aongezea adhabu kwa siku arobaini na tano kutumikia adhabu hiyo.
Shirikisho la soka ulimwenguni limeongeza muda wa adhabu na marufuku dhidi ya raisi wa chama cha soka nchini Ghana Kwesi Nyantakyi kwa siku arobaini na tano zaidi.
Kwesi alipigwa marufuku mnamo tarehe nane mwizi wa sita mwaka huu kwa siku tisini na mahakama ya Kamati ya Maadili ya Fifa ya kujitegemea.
Kamati hiyo inafanya uchunguzi rasmi dhidi ya Nyantakyi baada ya kupigwa picha za video kwa siri akipokea zawadi ya fedha tasilimu .
Nyongeza ya adhabu itaanza kutekelezwa mara moja mnamo tarehe sita ya mwezi huu.Ikumbukwe kwamba Nyantakyi alirekodiwa katika uchunguzi wa siri na mwandishi wa habari machachari
Kutoka nchini Ghanaian Anas Aremeyaw Anas taking anaonekana akipokea kitita cha dola elfu sitini na tano sawa na paundi elfu arobaini na nane kutoka kwa mwandishi mwingine wa habari aliyejifanya ni mfanyabiashara .
Baadhi ya vipande vya video hiyo kutoka kwa Anas baadaye vilirushwa hewani na idhaa ya BBC World Service katika makala ya kiuchunguzi iliyopewa jina la Africa Eye.
Baada ya marufuku ya awali, mnamo tarehe nane June Nyantakyi alichukua uamuzi wa kujiuzulu wadhifa zake kama mjumbe wa bodi wa bodi ya shirikisho la kimataifa , Fifa, na pia nyadhifa zake katika Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).
Alichia ngazi katika baraza la Fifa Council na pia kujiweka pembeni katika nyadhifa zake katika shirikisho la Caf ikiwemo nafasi ya makamu wa kwanza wa raisi ,nafasi ya juu zaidi kama kiongozi mwandamizi katika shirikisho hilo baada ya rais wake.
Nyantakyi amekuwa akikana makosa yake .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.