Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Azindua Tamasha la Urithi Festival

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Tamasha la Urithi (Urithi Festival) katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo ya Nguli wa Sanaa za Ngoma ya Urithi Festival mwaka 2018 Mjukuu wa Mzee Morris Nyunyusa kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kutunza na kudumisha utamaduni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa kwa mikono na kikundi cha Eddie Collection wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi (Urithi Festival) kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.