Habari za Punde

Tetesi za Soka Ulaya : Ronaldo, Pogba, Mourinho, Southgate, Mina

Mchezaji Cristiano Ronaldo akiwa katika ubora wake uwanjani.
Meneja wa Manchester United ameishauri klabu hiyo isimsaini mshambuliaji Cristiano Ronaldo msimu ujao. Mchezaji huyo miaka 33 alihamia Juventus kutoka Real Madrid. Sunday Mirror)
Mourinho anasema alijua kuwa msimu huu ungekuwa mgumu sana kwa Manchester United. (Daily Star Sunday)
Mchezaji wa Kimataifa Paul Pogba.
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 25, anasema anataka tena kujaribu kujiunga na Juventus mwezi Januari kutokana na kuendelea kudhoofika kwa uhusiano wake na Mourinho. (Tuttosport, via Manchester Evening News)
Aliyekuwa nahodha wa Liverpool Graeme Souness anasema kiungo wa kati Pogba yuko tu kwenye klabu kuweza kudumisha thamani yake hadi United ipate kumuuza. 
Neymar
Aliyekuwa mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, anawez kuhamia Arsenal au Chelsea ikiwa angeamua kuhamia Ligi ya Premia kwa sababu anapenda London. (Sunday Express)
Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele, 31, anaweza kuondoka klabu hiyo Januari kijiunga na ligi ya China ya Chinese Super League, klabu ya Sinobo Guoan kwa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya paunia 192,000 kwa wiki. (Sun on Sunday)
Mousa Dembele.
Kiungo wa kati wa Spurs Eric Dier, 24, anatetea hatua ya klabu ya kutomsaini yeyote msimu ulioipita na kusema kuwa wana kikosi kizuri. (Mail on Sunday)
Meneja wa England Gareth Southgate hawezi kualikwa na malkia kwa sababu serikali huzuia tuzo kwa watu ambao hawalipi ushuru. (Sunday Times)
Jack Wilshere.
Kiungo wa kati wa West Ham Jack Wilshere hayuko katika kiwango cha kumwezesha kujumuishwa kwenye kikosi cha England na Southgate anasema mchezaji huyo wa miaka 26 ni lamzima aanze kucheza vizuri ikiwa anataka kucheza mechi ya kimataifa. (Sunday Telegraph)
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amekana kwamba amekosana na kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, lakini anasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anahitaji kucheza maeneo tofauti katika klabu hiyo.. (Guardian)
Unai Emery.
Manchester United haijakiubaliana kuhusu mkataba mpya wa kumzuia mshambuliaji wake Anthony Martial ,22, kuondoka katika uwanja wa Old Trafford , huku raia huyo wa Ufaransa akiendelea na mazungumzo na klabu hiyo.(Goal)
West Brom ilifeli kumnunua kiungo wa kati wa Blackburn Rovers na Uingereza Bradley Dack, 24 kwa dau lililovunja rekodi la £15m. (Sun).
Anthony Martia
Everton imekataa dau la muda wa mwisho la £25m kutoka RB Leipzig kumnunua mshambuliaji Ademola Lookman, 20, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka kumnunua raia huyo wa Uingereza kurudi katika uwanja wa Red Bull Arena. (90min)
Jurgen Klopp amemuonya kipa wa Liverpool Simon Mignolet, 30, kuwa tayari kuchezeshwa baada ya kipa mpya Alisson. Raia huyo wa Ubelgiji sasa atachezeshwa baada ya kipa Alisson. (Mirror)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.