Habari za Punde

Timu ya JKU Imetangazwa Bingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kwa Mwaka 2017/2018 Baada ya Kuifunga Timu ya Jamuhuri Kwa Bao 3 -1 Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

 Mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri akimpita Beki wa Timu ya JKU wakati wa mchezo wao wa kufunga Michuano ya Ligi ya Nane Bora Zanzibar mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya JKU imefanikiwa kilitetea Kombe hilo la Ubingwa wake na kuibuka mshindi wa mabao 3-1 na kutangazwa rasmin kuwa Bingwa kwa Mwaka wa 2017/2018 katika Ligi Kuu ya Zanzibar.
Katika mchezo huo umeonesha upizani wa hali ya juu kutokana na wachezaji wa Timu ya Jamuhuri kuonesha kiwango cha juu cha mchezo katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Timu ya JKU imeandika bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Ponsiana Malik katika dakika ya tatu ya mchezo huo kipindi cha kwanza. 
 Bao hilo la timu ya JKU limeamsha mori kwa timu ya Jamuhuri na kulishambulia lango la timu ya JKU kupitia washambuliaji wake lakini haikuwa bahati yao katika kipindi hichi Timu ya JKU imeandika bao lake la pili kupitia mshambuliaji wake Mbarouk Chande kuandika bao hilo katika dakika ya kumi na moja ya mchezo huo.
Nao Timu ya Jamuhuri ilibidi kuzinduka katika uzingizi na kulishambulia lango la JKU na kufanikiwa kuandika bao lake la kwanza kupitia mshambuliaji wake Khamis Abdulrahaman katika dakika ya 36 ya mchezo huo kipindi cha kwanza.
JKU wamefunga karamu hiyo ya mabao katika dakika ya 63 kuandika bao lao la tatu kupitia mshambuliaji wake Salum Mussa.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.