Habari za Punde

Video - Waziri wa Mambo ya Ndani Awataka Jeshi la Polisi Kuvitumia Vizuri Vya Barabarani.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, KANGI LUGOLA ameliagiza Jeshi la Polisi kuvitumia vizuizi vya barabarani katika kuimarisha Ulinzi na kuzuia uhalifu badala ya kuwa chanzo cha rushwa na kero kwa wananchi.
Waziri LUGOLA ametoa agizo hilo wilayani KAKONKO leo wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Uslama ya Mkoa wa KIGOMA mara baada ya kuwasili mkoani humo na kusema pamoja na lengo zuri la vizuizi vya barabarani lakini wawe makini katika utekelezaji wa kazi zao ili wasikinzane na ilani ya CCM inayoelekeza kuwapunguzia kero wananchi na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.