Habari za Punde

Zoezi la kusajili wakaazi wa Zanzibar katika mfumo kielektroniki (E ID Card) laanza katika Mkoa wa Kusini Unguja

 Zoezi la uandikishaji wananchi wa Zanzibari katika mfumo wa kidigitali limeanza rasmi leo Sept 8, 2018 katika Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja. Ambapo idadi kubwa ya wananchi imejitokeza kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho ya kielektroniki (E-ID CARD). Mapema wiki hii rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein alizindua Vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar na Uzinduzi wa Uimarishaji Mfumo wa Usajili kielektroniki hafla iliofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
Wananchi wakiendelea kuandikishwa.
Mwitikio wa wananchi ulikuwa ni mkubwa sana.
Wananchi wakingoja foleni ili kuingia katika chumba cha kuandikishwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.