Habari za Punde

Kimbunga Michael: Majimbo Matatu Kusini Mashariki Mwa Marekani Kuathirika

Takriban watu nusu milioni wanatakiwa kuondoka haraka katika makazi yao eneo la kusini mashariki mwa Marekani ili kukupisha kimbunga Michael ambacho kinakaribia kulikumba eneo hilo.
Taarifa za watabiri wa hali ya hewa zinasema kimbuka hicho kwa sasa kimekwisha ingia katika hatua ya tatu na kuongezeka kasi yake kwa kadri kinavyopitia ghuba ya Mexico kuelekea Jimbo la Florida,Alabama na Georgia.
Kimbunga hicho kinasababisha upepo mkali ambao unakwenda kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa,ambapo wataalam wanasema kuwa wakazi wa jimbo la Florida leo huenda watakumbwa na mawimbi maji yatakayotupwa nje na upepo huo kwa kimo cha urefu wa mita tatu jambo ambalo ni hatari hivyo wanatakiwa kuondoka maeneo yanayolengwa na kimbunga Michael.
Gvana wa jimbo la Florida Rick Scott, amekielezea kimbunga hicho kuwa ni hatari Zaidi.
Kutokana na hali hiyo majimbo ya Alabama, Florida na Georgia yametangaza hali ya hatari,ambapo Alabama maeneo 92 watu wake wanatakiwa kupisha madhara ya kimbunga hicho Michael kusini mwa jimbo la Georgia na maeneo 35 ya jimbo la Gergioa kimbuka hicho kinatarajiwa kuyafikia.
Naye Gavana wa Jimbo la Carolina ya Kaskazini Roy Cooper ameonya kwamba watu wake kwamba wanatakiwa kuchukua tahadhali kwani huenda madhara ya kimbunga hiki yakawa makubwa Zaidi ya Kimbunga Florence kilicholikumba eneo hilo mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.