Habari za Punde

Pangawe watakiwa kutunza miundombinu ya majli

Takdir Ali-Maelezo Zanzibar                                               
Wananchi wa Jimbo la Pangawe wametakiwa kuitunza na kuiendeleza Miondombinu ya maji iliyowekwa ili iweze kuwa endelevu na kufikia malengo yaliokusudiwa.
Akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kuimarisha huduma za maji Mwakilishi wa Jimbo hilo Khamis Juma Maalim amesema uongozi wa Jimbo umeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha tatizo la Maji linaondoka na kubaki kuwa historia.
Amefahamisha kuwa kiasi ya Visima tisa vimechimbwa na Uongozi wa Jimbo kwa kushirikiana na Taasisi ya Direct aid katika maeneo mbalimbali ya Jimbo ikiwa ni pamoja na Kinuni, Mnarani, Nyarugusu, Muembemajogoo na Pangawe hatua iliopunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la Maji kwa Wananchi.
Mwakilishi huyo amesema kitendo cha baadhi ya Wananchi kuiharibu kwa makusudi miondombinu ya maji hakileti picha nzuri na kuwaomba kila mmoja kuwa mlinzi kwa mwenzake.
Amefahamisha kuwa wanaofanya hujuma hizo hurudisha nyuma juhudi za viongozi katika kutatua matatizo ya Wananchi Jimboni humo.
“Sisi tunajenga wengine wanavunja hali hii haivumiliki hata kidogo, nakuombeni mukiwabaini tu wafikisheni katika vyombo vya Sheria ili wachukuliwe hatuwa na kupata funzo”,alisema Mwakilishi huyo.
Aidha amesema uongozi wa Jimbo hilo utaendelea kubuni mbinu zitakazoweza kulipatia ufumbuzi tatizo hilo na kuwaomba Wananchi kushirikiana nao kwa hali na mali.
Kwa upande wake Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Magharib “B” Thuwaiba Jeni Pandu amesema wamejipanga kutatua matatizo ya Wananchi hatua kwa hatua kulingana na vipao mbele walivyoweka Wananchi wenyewe.
Amewataka Wananchi kuwa na ustahamilivu kwani matatizo yanayowakabili katika Jimbo lao ni mengi na kuwataka kila mmoja kutimiza wajibu wake kulingana na nafasi alionayo.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.