Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu Atoa Taarifa Kuhusiana na Kusogezwa Mbele Hadi Jioni Utiaji Saini Mkataba wa Mgawayo wa Uzalishaji Mafuta na Gesi Asilia

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa taarifa ya hafla ya Utiaji wa Saini ya Mkataba wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na RAKGAS, inayotarajiwa kufanyika jioni katika viwanja vya Ikulu Zanzibar na kuhudhuriwa na Mtawala wa Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al-Qasimi.na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein. 
Wageni waalikwa pamoja na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria hafla ya utiji wa saini inayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria hafla ya utiaji wa saini wa  Mkataba wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na RAKGAS, inayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wageni waalikwa wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee akibadilishana mawazo na Viongozi wa Kampuni ya RAKGAS L.L.C, baada ya kuhairishwa kwa sababu maalum mpaka jioni leo baada ya kuwasili kwa Mtawala wa Ras Al Khaiman.


Brass Band ya Jeshi laPolisi Zanzibar wakiburudisha Wageni waalikwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.