MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza katika
kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga
akisikiliza kwa umakmini hoja mbalimbali kwenye kikao hicho
NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Mohamed Haniu akipitia kabrasha
wakati wa kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo Alhaj
Mustapa Selebosi
Awali hospitali hiyo ilitarajiwa kujengwa katika kata ya
Masiwani ambapo tayari jengo la utawala la ghorofa moja lilikwisha
jengwa ambalo linadaiwa kugharamia kiasi cha shilingi Milioni 700.
Mjadala uliibuka ndani ya kikao hicho cha baraza hilo ambapo
madiwani walipingana eneo gani linaweza kuwa sahihi kwa ajili ya
ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo mchakato wake unadaiwa kuanza tangu
mwaka 2005.
Akizungumza Mwenyekiti wa baraza hilo Mstahiki Meya Mustafa Seleboss
alisema kweli yapo maeneo matatu yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa
hospitali hiyo ambayo kila eneo linachangamoto zake huku akibainisha
umuhimu wa hospitali hiyo kujengwa katika eneo hilo la Mwakidila.
Aidha alisema Halmashauri imekwisha pokea kiasi cha shilingi Milioni
500 kati bilini 1.5 toka Serikali kuu kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa
hospitali hiyo ambayo itaondoa sitofahamu ya kutokuwepo kwa Hospitali
hiyo ndani ya Wilaya.
Seleboss alisema hakuna haja ya kuendeleza malumbano juu ya wapi
Hospitali hiyo itajengwa huku fedha hizo zikiwa zimetolewa na Serikali
kwa mashari ya utekelezaji wa haraka wa ujenzi wa hospitali hiyo
ambayo itapunguza msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo.
“labda niwaeleze ukweli ndugu zangu madiwani plani ya ujenzi wa
Hospitali ya Wilaya eneo la masiwani lipo palepale ila kutokana na
mgogoro uliopo wa ardhi tunalazimika fedha hizo kuanza kujenga
Mwakidila badala ya masiwani”Alisema Seleboss.
Hata hivyo aliwanasihi madiwani na wananchi wa kata ya masiwani
ambao walitarajia kupata hospitali hiyo ya Wilaya kuwa ndoto hiyo
haijafutika na itajemgwa Hospitali nyingine kwa kupitia fedha toka
vyanzo vya ndani vya Halmashauri.
“Tulikuwa na maeneo matatu ya mwakidila,masiwani na kihongwe
lakini kutokana na changamoto ya maeneo hayo mawili ya kihongwe na
masiwani tumeona ni bora mradi huu tuuelekeze mwakidila eneo lililopo
karibu na barabara kuu ya Tanga-Pangani”Alisema.
Awali akizungumzia mkanganyiko huo Diwani wa kata ya Duga Khalid
Rashid(CUF) alisema hapingani na maamuzi ya baraza lakini jambo la
msingi ni kuangalia gharama zilizotumiaka eneo la masiwani za ujenzi
wa jengo la ghorofa moja la utawala kwa ajili ya Hospitali ya
Wilaya.
Alisema ipo haja kwa Halmashauri kuwa makini juu ya taarifa za
wataalamu ambao awali waliishauri Halmashauri kujenga Hospitali hiyo
eneo la masiwani ambapo zaidi ya shilingi milioni 700 zimetumika
katika ujenzi wa jingo la utawala.
“Mstahiki Meya sipingi na wala sikatai hospitali hiyo kujengwa
mwakidila lakini tuwe makini na wataalamu wetu tumewekeza fedha nyingi
kwa nini hizi bilioni 1.5 zisiendeleze pale masiwani? lakini ni
maamuzi ya baraza wacha tuyaheshimu”Alisema Rashidi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapa alisema kumekuwepo
na maneno ya fitina juu ya mradi huo wa Hospitali lakini jambo muhimu
muafaka umefikiwa wa wapi itajengwa hilo ndio jambo la msingi.
Alisema hakuna haja ya kulumbana hasa katika maswala ya msingi
na maendeleo ya wanachi makubaliano ndio jambo muhimu ili pande zote
mkubaliane kwa pamoja wapi hospitali hiyo itajengwa na lengo ni
kumsaidia mwananchi katika swala la afya.
No comments:
Post a Comment