Habari za Punde

MAZOEZI YA PAMOJA YA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMEWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI


WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga mazoezi ya  ya mafunzo ya Ushirikiano Imara mwaka 2018 ya Kijeshi kwa vikosi vya
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki  kwenye eneo la Mlingano wilayani Muheza mkoani Tanga ambayo yalikuwa na malengo ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi,uharamia,majanga na kujenga uchumi imara katika nchi
Waziri wa Ulinzi wa  Kenya Balozi Raychelle Omamo akitoa salamu kwenye ufungaji huo wa mafunzo


Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo akizungumza katika halfa ya ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyifanyika kwenye eneo la  Mlingano wilayani Muheza Mkoani Tanga

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi kushoto akiwa na  Waziri wa Ulinzi wa  Kenya Balozi Raychelle Omamo
 Vikosi mbalimbali vikipita mbele ya mgeni rasmi leo 


 MAJESHI ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yapo imara kupambana na vitendo vya uvunjifu wa amani katika nchi wanachama baada ya kuhitimisha mazoezi ya pamoja yaliyozikutanisha nchi hizo mkoani Tanga .

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ulinzi Dr Husein Mwinyi wakati wa kufunga mazoezi hayo ambayo yalikuwa na malengo ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi,uharamia,majanga na kujenga uchumi imara katika nchi wanachama.

Aidha Dkt Mwinyi alisema kumekuwepo na ufanisi wa hali ya juu wa utayari wa kukabiliana na majanga kama hayo hivyo jukumu lipo kwa vikosi hivyo kujiamini na kutumia mbinu walizopata ili kuzisaidia nchi zao.

“Tunaimani sasa baada ya mazoezi haya kwanza vikosi vyetu vitakuwa imara zaidi lakini ni wakati wa kuanza kupambana na matukio kama hayo si kwa nchi mojamoja bali kwa kushirikiana zaidi”Alisema Dr Mwinyi.

Mazoezi hayo yalizikutanisha nchi zote wanachama ikiwa pamoja na Tanzania ambae ni mwenyeji,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi huku Sudani kusini haikufika kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wao.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi toka Nchini Kenya Balozi Rachael Omamo alisema mbali ya kubadilishana uzoefu katika Nyanja ya kiusalama bali mazoezi hayo yanajenga mahusiano bora kwa Nchi zote wanachama.

Alisema Vikosi hivyo vinahitaji kujitathmini zaidi na kuitumia fursa hiyo kujiimarisha katika Nyanja zote ili kuweza kukabiliana na majanga yanayozikabili nchi hizo.

“Majeshi yetu yanatakiwa yavute soksi ili kujiweka imara na mambo mbalimbali yanayozikabili nchi zetu lakini lazima tushirikiane kwa kila hali na kufanya hivi tunaweza kufanikiwa na kuwa sehemu salama”Alisema Balozi Omamo.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Venance Mabeyo alisema mazoezi hayo yanajenga hasa kufahamiana katika vikosi hivyo na ndio msingi wa kufanikiwa katika mapambano dhidi ya majanga kwa nchi wanachama.

Alisema ni mazoezi yaliyoviongezea uwezo vikosi hivyo hasa na mapambano ya kigaidi,uharamia na majanga mbalimbali na hiyo ndio azma ya mazoezi hayo ambapo bado nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto ya mapambano hayo.

“Unajua lazima tujifunze mbinu za ugaidi na uharamia lakini lazima tufahamu watu wanaofanya matukio kama haya ni vikundi vidogovidogo ambavyo si rasihi kuvitambua na umoja wetu kupitia mazoezi haya lazima tutafanikiwa”Alisema Jeneral Mabeyo.

Jenerali Mabeyo mbali na hayo pia alizungumzia mwanajeshi wa Tanzania aliyeuwawa katika Nchi ya Demokrasia ya Congo akiwa katika majukumu ya kulinda amani alisema ni kweli na ni mapambano ya kawaida dhidi ya waasi hao.

Alisema ni ajali ya kawaida hasa kwa vikosi hivyo vinavyolinda amani katika nchi mbalimbali hapa Duniani na inaweza kutokea sa yoyote hivyo jukumu kubwa lililopo mbele ni kusahihisha makosa hayo.

“Ni tatizo na tunasahihisha lakini si jambo kubwa sana ni swala la kawaida katika maeneo ambayo wanajeshi wetu wapo kwa ajili ya kulinda amani katika nchi hiyo ya Congo”Alisema. 


Alisema wanajeshi wa Tanzania wapo nchini humo kusaidia kupamba na waasi kwa ajili ya kurudisha amani ambayo inaonekana kuyumba na jambo hilo husababishwa na vikosi vya waasi ambao wanapamba na majeshi ya Serikali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.