Habari za Punde

Serikali yaanza kufanya usajili wa watru weenye ulemavu nchini

Na Takdir Ali,                                                      12-11-2018.
Wananchi wametakiwa kulipa kipao mbele suala la Watu wenye ulemavu ili waepukane  matatizo yanyowakabili katika jamii.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye ulemavu Zanzibar Abeidah Abdallah Rashid alipokuwa akitoa maelezo kuhusiana na usajili katika Mkoa  wa Kusini Unguja.
Amesema Watu wenye Ulemavu wanakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo kukosa elimu hivyo iwapo wanajamii watashirikiana wataweza kusoma na kupata elimu kama Watu wengine.
Aidha amesema Serikali imeanzisha usajili kwa Watu hao ili kuweza kujuwa idadi na mahitaji yao na kuingizwa  katika mipango mbali mbali ya maendeleo.
Hata hivyo amelaani kitendo cha baadhi ya Watu waliokataa kusajiliwa na kusema ni kurudisha nyuma mipango ya maendeleo na kuwaomba kubadilika mara moja.
“Baadhi ya Watu wenye Ulemavu wanapita wakilalamika hawapati misaada yoyote lakini cha kushangaaza hawataki kusajiliwa hivyo nani atawafahamu na kuwasaidia.”.aliuliza Mkurugenzi huyo.
Sambamba na hayo amewataka kuachana na dhana potefu ya kuwa hata wakisajiwa hakuna lolote wanalolipata jambo ambalo halina ukweli ndani yake bali ni kurejesha nyuma mipango ya Serikali.
Amefahamisha kuwa  kuna baadhi ya Watu wenye ulemavu wamebuni  mipango ya kuanzisha miradi ya maendeleo lakini wanashindwa kutokana na kutokuwa na mitaji yakutosha na kuwaomba watu wenye uwezo kuwasaidia kwa hali na mali.
Mbali na hayo amewaomba Wakuu wa Mikoa,Wilaya na Masheha kuwashirikisha wenye ulemavu katika mipango ya Serikali ili wajihisi kuwa hawajatengwa na jamii na serikali Serikali yao.
Kwa upande wake Afisa wa Watu wenye ulemavu Mkoa wa Kusini Unguja Mabula Nalimi Machalila amesema zoezi la usajili katika Mkoa huo limekwenda vizuri ilicha ya matatizo madogo madogo yaliojitokeza ikiwemo baadhi ya Wananchi kukataa kusajiliwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.