Habari za Punde

Waziri Mwakyembe kufikisha Changamoto za Veta kwa viongozi Husika

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akitoa rai kwa washiriki wa Tamasha la Michezo na Maonesho ya Vyuo vya Ufundi  kutowaingiza wachezaji mamluki katika michezo mashindano hayo,leo Jijini Dodoma alipokuwa akizindua tamasha hilo linalofanyika katika Uwanja wa Jamhuri,wapili kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira Kazi Vijana na Walemavu Mhe.Anthony Mavunde na wakwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Kanda ya Kati Bw.Ramadhani Mataka.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira Kazi Vijana na Walemavu Mhe.Anthony Mavunde akitoa ahadi ya kusimamia umoja wa vyuo vya ufundi Dodoma leo katika uzinduzi wa Tamasha la Michezo na Maonesho ya Vyuo vya Ufundi yaliyoanza leo katika uwanja wa Jamhuri ambayo yatadumu kwa muda  wiki moja na wa pili kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe kutoka kulia wakwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Kanda ya Kati Bw.Ramadhani Mataka
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akitizama matofali ya (interlock) alipotembelea banda la Chuo cha Ufundi Don Bosco Dodoma katika Tamasha la Michezo na Maonesho ya Vyuo vya Ufundi  yaliyoanza leo   katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa Tamasha la Michezo na Maonesho  ya Vyuo vya Ufundi yaliyozinduliwa leo katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.              

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa chuo cha Veta kanda ya kati mara baada ya uzinduzi wa tamasha la michezo na maonesho ya vyuo vya ufundi yatakayofanyika kwa wiki moja katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, wapili kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira Kazi Vijana na Walemavu Mhe.Anthony Mavunde.

Na Anitha Jonas – WHUSM.12/11/2018.DODOMA.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi viongozi wa Veta kufikisha vilio  vya changamoto zao kwa viongozi husika.
Mheshimiwa Mwakyembe ameyasema hayo leo jijijni Dodoma  alipokuwa akizindua Tamasha la Michezo na Maonesho ya  vyuo vya ufundi Kanda ya Kati Dodoma,mara baada ya viongozi hao kusoma risala yao kuhusu tamasha lao ambalo litadumu kwa wiki nzima  lengo likiwa ni  kujenga umoja na kuboresha mahusiano kwa vyuo  vya ufundi pamoja na kuweka mikakati ya kutoa elimu bora yenye kusaidia taifa kufika malengo ya uchumi wa Kati na nchi ya viwanda.
“Kwanza ninawapongeza sana kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kuwajenga vijana wenye ujuzi ambao wanaelewa thamani ya michezo kwani michezo ni afya na michezo ni  ajira kwa hakika jambo hili mlilolifanya ni jambo  zuri na pia natoa rai kwenu wanamichezo wote mnaoshiriki michezo hii kucheza kwa amani ,“alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo Mhe.Mwakyembe alisisitiza kuwa katika mashindano hayo asingependa kusikia kuwepo kwa wachezaji mamluki ambao siyo wanamichezo kutoka katika vyuo husika vilivyoshiriki tamasha hilo.
Pamoja na hayo nae Naibu Waziri Ofisi ya Mkuu Ajira Kazi Vijana na Walemavu Mhe.Anthony Mavunde alieleza mipango mbalimbali serikali iliyojiwekea ya  kushirikiana na VETA kwa ajili ya kuhakikisha inawasaidia vijana  kupata mafunzo ya ufundi ambayo yatawawezesha kujiajiri na kufanikisha adhima ya nchi yetu kufikia uchumi wakati na nchi ya Viwanda.
“Kupitia umoja huu wa vyuo vya ufundi kwa kanda ya kati waliyouanzisha nitajitahidi kuwasimamia na kuhakikisha wanaanzisha kiwanda chao wenyewe cha mfano ,“Mhe.Mavunde.
Aidha,nae Kaimu Mkuu wa Chuo Veta Kanda ya Kati Bw.Ramadhan Mataka alieleza kuwa VETA kama wasimamizi wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi nchini hivi karibuni uongozi wa Kanda ya Kati imevifungia vyuo ishirini vilivyokuwa havina viwango vya kutoa mafunzo kukuzingatia sheria na utaratibu wa hadhi ya vyuo vya ufundi.
 “Kupitia Umoja wa Vyuo vya Ufundi tunataka tuunde mkakati madhubuti wa kuboresha kozi zetu na kuhakikisha tunatoa mafunzo yenye ubora  ambayo yatatusaidia wote kutembea katika njia moja kwa manufaa ya taifa letu na uchumi wa nchi  yetu,”Bw.Mataka.
Sambamba na hayo  Bw.Mataka alitoa rai kwa vyuo vyote vya ufundi vilivyopo Kanda ya Kati ambavyo havijasajiliwa vijisajili haraka ili kurasimisha shughuli zao,”Bw.Mataka
Halikadhalika nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyuo vya Ufundi Dodoma, Bw.Jeremia  Philip alieleza kuwa umoja huo unamalengo mbalimbali ikiwemo kuboresha masomo ya mafunzo ya ufundi na kuwaongezea vijana ujasiri wa kujiajiri mara baada ya kufuzu masomo yao.
 Pamoja na hayo Bw.Jeremia alieleza kuwa umoja huo umeanzisha mpango wa kurudisha darasani vijana ambao hawakupata elimu waliyochini ya miaka kumi na tano wa kuwapeleka darasani  na kuwapatia mafunzo ya ufundi kwa lengo la kuwasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.