Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed Atembelea Miradi ya Maendeleo Kisiwani Pemba.

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed, akichungulia chemchemu ya maji katika kijiji cha Kisima Pemba Tondooni Wilaya ya Micheweni, ambayo imehifadhiwa na kupitia mradi wa Kaya Masikini shehia hiyo ili maji yasipotee na kupata maji safi na salama
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed, akipata maelezo juu ya Chemchemu ya Maji Tondooni Wilaya ya Micheweni, kutoka mkuu wa Ufundi wa Mamlaka ya maji ZAWA Pemba, Juma Othaman wakati alipotembelea Chemchemu hiyo kujuwa sababu ambazo wananchi bado hawapati maji ipasavyo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed, akiakagua ujenzi wa nyumba ya makaazi ya Makamu wa Pili unavyoedelea katika kijiji cha Pagali Wilaya ya Chake Chake.
(Picha na Abdi Suleiman - Pemba.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.