Habari za Punde

Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Afanya Ziara Kutembelea Studio ya Rahaleo.

Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume na Viongozi wenzake wakipatiwa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Studio ya Muziki na Filamu Zanzibar kutoka kwa Meneja wa Studio hiyo Abeid Mfaume Faki alipotembelea Studio hizo Raha leo mjini Zanzibar.
Mhariri Picha za Video katika Studio ya Muziki na Filamu Zanzibar Mohamed Abdulrahman akionyesha kazi wanazozifanya katika Studio hio kwa Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume na Viongozi wa Wizara hiyo.
Mhariri Picha za Video katika Studio ya Muziki na Filamu Zanzibar Mohamed Abdulrahman akionyesha kazi wanazozifanya katika Studio hio kwa Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume na Viongozi wa Wizara hiyo.
Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume na Viongozi wenzake wakipatiwa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Studio ya Muziki na Filamu Zanzibar kutoka kwa Meneja wa Studio hiyo Abeid Mfaume Faki alipotembelea Studio hizo Raha leo mjini Zanzibar.
Vijana wakimsikiliza Naibu Waziri wa Vijana, Utamaduni  Sanaa na Michezo Lulu  Msham Abdalla alipofanya mkutano nao katika studio ya Wasanii Rahaleo
Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
Na.Khadija Khamis -Maelezo Zanzibar.
Imeelezwa kuwa Vijana ni hazina  ya Taifa hivyo iko haja ya kubadilika na kujitambua kwa  kuweza kubuni miradi mbali mbali katika Shehia na Wilaya zao ili  iweze kuwapatia maendeleo yao .
Hayo aliyasema Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana  Utamaduni, Sanaa na Michezo Lulu Msham Abdalla  wakati wa kikao cha Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo na Viongozi wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka kila Wilaya ya Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Wasanii Rahaleo.                                                                                                           Alisema vijana wanatakiwa kuwa wabunifu kwa kuandaa mradi mkubwa katika kila  wilaya ili uwe chanzo katika kusaida miradi midogo midogo itakayoanzishwa ndani ya shehia na kuwaletea maendeleo.
Alisema nia na madhumuni ya Wizara ya Vijana ni kuwakomboa  vijana kutoka sehemu moja kwenda nyengine kwa lengo la kuhakikisha wanajiimarisha katika kupata ajira  na kujikwamua na umasikini .
Aidha alisema Wizara imetenga zaidi ya shilingi billion tatu kwa ajili ya miradi ya vijana katika wilaya zote za Unguja na Pemba ili kuhakikisha lengo la Serikali la kuwakomboa vijana katika kukuza maendeleo linafikiwa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Amour Hamil Bakari alisema mfumo mzima wa Baraza la Vijana bado linaonyesha halijakaa vizuri  hivyo ipo haja ya kutumia busara kuliimarisha liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Alieleza kuwa lengo la Serikali ni kuona viongozi wanashirikiana na wanachama wenzao na watendaji wengine kutekeleza miradi watakayoanzisha kwa  kiushindani .
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana  Zanzibar Khamis Rashid  Kheir alisema Baraza la vijana lilikuwa linakabiliwa na changamoto nyingi lakini jambo muhimu kwa sasa ni  Wizara kushirikiana pamoja na Vijana ili kuona malengo ya kuwepo Mabaraza hayo linafikiwa.
Aidha alisema Serikali inania njema ya kusaidia juhudi za Vijana zinaimarika na kuhakikisha wanapata maendeleo kupitia miradi mbali mbali inayoanzishwa kuanzia ngazi ya Shehia, Wilaya hadi Mkoa .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.