Habari za Punde

TTCL Yasaini na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Kupeleka Huduma Vijijini.


Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) mara baada ya kuweka saini katika mkataba wa kusambaza mawasiliano maeneo ya vijijini leo jijini Dar es Salaam. Katikati wakishuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Issack Kamwele pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dk. Maria Sasabo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akisaini mkataba na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga (kushoto waliokaa) leo jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo TTCL itasambaza mawasiliano maeneo ya vijijini ili kuchochea maendeleo. Wanao shuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Issack Kamwele pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dk. Maria Sasabo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Issack Kamwele akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini na watendaji wakuu wa kampuni za simu zilizoshinda zabuni ya UCSAF na watendaji wa mfuko huo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Issack Kamwele (kulia mbele) akizungumza na watendaji wakuu wa makampuni ya simu yalioshinda zabuni ya UCSAF kusambaza mawasiliano vijijini pamoja na watendaji wa mfuko huo.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akibadilishana nakala ya mkataba na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga (kushoto) mara baada ya kutiliana saini leo jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo TTCL itasambaza mawasiliano maeneo ya vijijini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuelezea shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza zabuni hiyo kwa ufanisi.

 

Picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Issack Kamwele mara baada ya hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.