Habari za Punde

WATANZANIA WANAOSOMA NCHINI CHINA WATAKIWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO NCHINI


Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki akizungumza katika mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi Watanzania Wanaosoma China- TASAFIC

Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki akiingia kwenye  Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi Watanzania Wanaosoma China- TASAFIC
Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania, Ndg Lusekelo Gwassa- ambaye ni Kaimu-Mwambata Elimu na Mwambata wa Uchumi Ubalozi wa Tanzania nchini China
Akisalimia Wahudhuriaji katika Mkutano Mkuu TASAFIC

 Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watanzania Nchini China Victoria Mwanziva

Akiwa na Thomas Mwabobo Katibu wa Jumuiya ya Watanzania wanaosoma Fushun
 Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Shenyang wakifurahia suala mkutanoni 

Salma Pazi (Mwenye Miwani) na Lisa Severin
 Wanafunzi Wakitanzania Wanaosoma China katika miji mbalimbali, wakisikiliza kwa umakini uwasilishwaji wa mada mbalimbali kwenye Mkutano Mkuu wa Watanzania wanaosoma China


 Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watanzania wanaosoma China akiongoza Kipindi cha Maswali na Majibu ambapo Wanafunzi Watanzania walipewa nafasi kuuliza masuala mbalimbali na kupata majibu na maelezo ya papo kwa hapo kutoka kwa Mheshimiwa Balozi[

 Picha ya Pamoja ya Viongozi wawakilishi wa Watanzania wanaosoma Majimbo Mbalimbali China nzima Waliohudhuria mkutano mkuu wa Watanzania wanaosoma China
Makamu Mwenyekiti wa Jimbo la Henan- Ibrahim Nyanza akipokea cheti cha uwakilishi kutoka kwa Mheshimiwa Balozi Kairuki

WATANZANIA wanaosoma nchini Chini wametakiwa kuwa chachu ya maendeleo, ubunifu, kujituma na kujitolea kwa manufaa ya Taifa la Tanzania ikiwemo kuchangamkia fursa za kimaendeleo.
 

Hayo yalisemwa Desemba Mosi mwaka huu na Mgeni rasmi wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi Watanzania Wanaosoma China- TASAFIC, Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki ambapo aliwataka pia kutanguliza uzalendo ili kuweza kujifunza kwa umakini.

Alisema watanzania wanaosoma nchini China juu ya masuala Tambuka haswa ya Kielimu, Kiutaratibu, Kinidhamu, Fursa mbalimbali na jukumu lao la kuwa chachu ya maendeleo, ubunifu, kujituma na kujitolea kwa manufaa ya Taifa letu. 

Mkutano huu uliandaliwa na Shirikisho la Watanzania Wanaosoma China na Ubalozi wa Tanzania Nchini China Ulileta pamoja Watanzania wanaosoma katika miji mbalimbali China kama Beijing, Dalian, Fushun, Jilin, Jinzhou, Harbin, Henan, Nanjing, Tianjing na Wenyeji wa Mkutano Shenyang.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.