Habari za Punde

Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar Yakamilika Katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Kikundi cha Vijana wakiongozwa na Picha za Marais wa Zanzibar kikifanya onyesho la mwisho la kuyaongoza Maandamano yatakayofanyika katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi hapo Uwanja wa Gombani Chake Chake Pemba.
Kikosi cha  Bendera kitakachoongoza Gwaride Rasmi la Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi kikifanya vitu vyake katika Uwanja wa Michezo wa Gombani wakati wa matayarisho ya Mwisho.
Moja ya Vikosi vya Ulinzi vitakavyoshiriki kilele cha maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi kikosi cha KMKM kikipita mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Gombani Chake Chake.
Vijana wa Halaiki wakifanya matayarisho ya mwisho kwa ajili ya  kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi hapo Uwanja wa Gombani Chake Chake Pemba.
Baadhi ya Vijana waliohamasika na matayarisho ya mwisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyokuwa yakifanyika katika Uwanja wa Michezo wa Gombani.
Balozi Seif  akisisitiza umuhimu wa Wajumbe wa Kamati za Sekriteriet ya Kamati ya Sherehe kuwajibika kwa majukumu yaliyombele yao katika kipindi hichi ambacho Kamati kuu haitakutana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiongoza Kikao cha Kamati hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa wakitafakari na kuchambua hitilafu ndogo ndogo zilizojitokeza wakati wa maandalizi ya mwisho ya Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi hapo katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri {VIP} Uwanja wa Gombani.

Na.Othman Khamis OMPR.
Siku adhimu na muhimu  ya kumbukumbu ya Historia ya Visiwa vya Zanzibar iliyoleta Ukombozi wa Waafrika wa Zanzibar kupitia Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 imewadia  kutimia Miaka 55 ifikapo Jumamosi ya Wiki hii ya Tarehe 12 Januari.
Matayarisho takriban yote yaliyofanywa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe hizo yamefikia ukingoni ambapo Kilele chake kitafikia katika Uwanja wa Michezo wa Gombani Chake Chake Pembe wakati washiriki wote wa Maadhimisho hayo wameshawasili Kisiwani Pemba.
Gwaride Rasmi la Vikosi vya Ulinzi na Usalama vitakavyopamba Maadhimisho ya sherehe hizo limekamilisha matayarisho yake yaliyoshuhudiwa na Wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar ikiongozwa na Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Raha iliyoje kwa Wananchi watakaoshiriki maadhimisho hayo kutokana na ukakamavu mkubwa uliyoonyeshwa na Vikosi hivyo kwenye matayarisho hayo ya mwisho ambayo imeonyesha muelekeo wa kufana.
Mbali ya gwaride hilo Sherehe hizo kama kawaida yake pia zitajumuisha Maandamano, Vikundi vya Utamaduni kutoka Wilaya mbali mbali Nchini pamoja na Vikundi vya Ulinzi vya Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} na kile Maalum cha Polisi Tarbushi.
Wakifanya tathmini ya Maandalizi hayo ya Mwisho katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri {VIP} ya Uwanja wa Michezo wa Gombani, wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa wameelezea kuridhika na hatua ya maandalizi hayo iliyofikiwa na washiriki wa Sherehe hizo.
Kilele cha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar Cha Januari 12 kitatanguliwa na Mkesha wa Maadhimisho hayo utakaojumuisha Ngoma za Utamaduni zitazoambatana na Fash Fash katika Uwanja wa Michezo waTibirinzi Chake Chake Pemba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikumbusha na kuhimiza washiriki wa Sherehe hizo wakazingatia utaratibu wa muda uliowekwa  ili ratiba iende kwa wakatyi uliopangwa.
Balozi Seif  alisema kwa vite Wajumbe hao hawatokutana tena kipindi hichi cha kukaribia maadhimisho ya sherehe hizo za Mapinduzi  aliwataka wajumbe wa Kamati zote kauhakikisha kwamba wanatekeleza ipasavyo majukumu yao waliyopangiwa  kwa lengo la kuweka sawa changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza kipindi hichi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.