Na Takdir
Ali, 7-01-2019.
Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt,Khalid Salum Muhammed amesema serikali
imeweka mikakati ya kuhakikisha mapato ya serikali yanaongezeka na kuziba
mianya yote inayoashiria kuvuja kwa mapato.
Amesema ukusanyaji wa mapato ni nzuri lakini bado kuna
baadhi ya watu
wachache wananakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na kuwataka wenye tabia
hizo kuacha mara ili kujiepusha na matatizo yanayojitokeza.
Ameyasema hayo huko Bandarini Malindi mara baada ya kumaliza ziara
iliowashirikisha Waziri Wa Fedha Na Mipango,Waziri Wa Biashara Na Viwanda Na
Waziri Wa Ujenzi,Mawasiliano Na Usafirishaji kufuatia kuibuka malalamiko katika
Baraza La Biashara ambapo mwenyekiti wake ni Raisi Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa
Baraza La Mapinduzi Dkt Ali Muhamed Shein.
Amesema walipofanya baraza la pili la biashara viongozi wa taasisi
binafsi walizungumzia matatizo ya uendeshaji wa bandari,miondombinu duni,na
kutoingia kwa makontena kutoka mombasa mamboa ambayo yanpaswa kupatiwa ufumbuzi
wa haraka ili kuwaondoshea usumbufu wananchi.
Amesema ziara hiyo imekuja kufuatia raisi wa zanzibar kuzitaka taasisi
zote zinazohusika wakutane na wafanyabiashara ili tatizo hilo liweze kupaiwa
utatuzi wa haraka sana.
Hata hivyo amewataka watendaji hao kutokubali kurubuniwa na baadhi ya
watu wachache wasioopenda maendeleo ya nchi na kutoa wito kwa wenye tabia hiyo
kuacha mara moja.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Mawasiliano Na Usafirishaji Dkt.Sira
Ubwa Mwamboya amesema mategemeo ya serikali yapo mikononi mwao hivyo ni vyema
kufanya kazi kwa ukweli ili kuweza kukusanya mapato vizuri na kuiwezesha
serikali kuhudumia vizuri wananchi wake.
Amesema wafanyabiashara wanakuwa wanaangalia maslahi katika biashara zao
hivyo nio vyema kutoshirikiana na wafanyabiashara wasiokuwa waamini fu ili
kuepukana na ubadhirifu unaoweza kujitokeza.
Nae Naibu Kamishna Wa Mamlaka Ya Mapato Zanzibar (Tra) Mcha Hassan Mcha
ameahidi kuyafanyia kazi maagizo waliopewa ili kuhakikisha mapato ya serikali
wanayokusanya yanaongezeka.
No comments:
Post a Comment