Habari za Punde

*WAJASILIAMALI WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI* *~ Ni kwa kuwaletea Vitambulisho vya Wajasiliamali wadogo* *~Gavana Shilatu awaonya Wafanyabiashara wakubwa*

Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Wajasiliamali wadogo wa Kata ya Kitama wamemshukuru Rais Magufuli kwa Kuja na majawabu ya changamoto zao hususani suala la kutozwa Kodi kubwa isiyoendana na mitaji wala mauzo yao.

Wajasiliamali hao wameyasema hayo mbele ya Afisa Tarafa Mihambwe, Gavana Emmanuel Shilatu wakati alipoenda kutoa elimu na hamasa juu ya vitambulisho vya Wajasiliamali wadogo.

*"Naomba Afisa Tarafa utufikishie salamu zetu kwa Rais Magufuli, mueleze sisi Wajasiliamali wadogo hatuna cha kumlipa kutokana na kuendelea kutupigania tufanye biashara zetu kwa amani na kwa faida. Hivi vitambulisho tumevipokea kwa mikono miwili maana ni mkombozi wetu"* alisema Mjasiliamali mdogo mmojawapo.

Akizungumza kwenye mkutano huo Gavana Shilatu alipiga marufuku Wafanyabiashara wakubwa ama Watu wasio wajasiliamali kuchukua vitambulisho hivyo.

*"Hivi vitambulisho havitolewi kwa Wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa zaidi ya Tsh. Milioni 4 ama kwa Watu wasio wajasiliamali, Ni marufuku kabisa. Hivi vitambulisho tuwaachie wajasiliamali wadogo wenye mitaji midogo ili nao wapate fursa ya kukua wawe wajasiliamali wakubwa"* alisema Gavana Shilatu.

Leo Jumamosi Januari 5, 2019 Gavana Shilatu alitoa elimu na hamasa kwa Wajasiliamali wadogo wachukue vitambulisho hivyo kwa kata za Kitama na Miuta na mwitikio ulikuwa mkubwa sana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.