Habari za Punde

TAMWA yazindua mwongozo wa wanawake kushiriki masuala ya Uongozi

Hawa Abdallah,ZANZIBAR

Vyama vya siasa,Viongozi wa dini, wanaume na wanawake wametakiwa kuona umuhimu wa kumpa mwanamke nafasi ya uongozi, aonekane kama ni mshiriki halali katika maswala ya kisiasa.

Hayo yamezungumzwa leo katika Ofisi za chama cha Waandishi wa habari Tanzania, Zanzibar (Tamwa Zanzibar) wakati wa kuzindua mwongozo wa wanawake kushiriki katika maswala ya uongozi.

Mwongozo huo ambao utatumika katika kuhamasisha makundi mbalimbali umevitaja vyama vya siasa, viongozi wa dini, wanaume na wanawake kuwa ni makundi ambayo yanatumika kurejesha nyuma wanawake kushiriki nafasi za uongozi hususani kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020.

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar DK Mzuri Issa alisema muongozo huo umeweza kuonesha hulali wa  mwanamke kushiriki katika nafasi za uongozi kidini, kijamii na kisiasa pamoja na umuhimu wa mawanamke  kushikilia nyadhifa mbalimbali za uongozi.

Aidha alisema muongozo huo umewaomba wadau mbalimbali kutumia nafasi zao kuhamasisha wanawake ambapo umewataka vyama vya siasa kuweka mkakati maalum kuanzia sasa, viongozi kutumia majukwaa yao mbalimbali ili kuelimisha na wanawake kuunga mkono wanawake wenzao.

Alisema ya wanawake katika Uchaguzi wa ushindani bado ni mdogo ambapo kwa Zanzibar wajumbe wa Baraza la wawakilishi ni sita kati ya 54, wabunge ni watatu kati ya 50 na madiwani ni 23 kati ya 111.

Akizindua muongozo huo Bodi ya TAMWA Rukia M Issa alisema vyama vya siasa vione umuhimu wa kumpa nafasi ya uongozi mwanamke kwa kumteua kuanzia ngazi ya chini.

Alisema baadhi ya wanaume wanaawacha wake zao pale mwanamke anapotangaza ile nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika maswala ya siasa.

Aidha aliwataka waandishi wa habari kuelekea uchaguzi 2020 izidi kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mwanamke kugombea katika nafasi ta uongozi.


Kwa upande wake kiongozi wa Dini Padri Essan Mlecha kutoka kanisa la mkunzini akichangia hoja ya mwanamke katika kuogombe nafasi ya uongozi alisema kuwa changamoto kubwa ipo katika uteuzi wa wagombea kupitia vyama vyao.

Alisema wanawake wengi hawapewi fursa ya kugombea katika vyama vyao hususani kuanzia ngazi ya chini ya uteuzi wa nani atasimama katika jimbo.

Aliwashauri viongozi wa siasa kuhakikisha wanawateua wanawake kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na uwakilishi na pasipo wakati majina yao yao katika uchaguzi wa 2020.

Akiwasilisha mada yaliyomo katika muongozo huo Meneja mtetezi wa Tamwa Hawra Shamte alisema jamii bado haijawa tayari nafasi za uongozi jambo ambalo linarejesha nyuma katika juhudi zao.

Alisema bado wanawake wapo nyuma katika uongozi na hii inatokana na kukatishwa tamaa na wanawake wenzao.

Aidha alisema jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa  ili kuona wanawake wanajitokeza na kuogombania  nafasi za uongozi katika chaguzi mbalimbali.

Katika uzinduzi huo ambao  umefanyika katika ukumbi wa ofisi ya TAMWA Tunguu
uliwashirikisha waandishi wa habari, Viongozi wa Dini, pamoja na wanasiasa.

Muongozo huo wa mwaka mmoja kuhamasisha wananchi kukubali uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi ambao baadae  utathminiwa umeshirikiana na TAMWA Zanzibar, Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) jumuiya ya waandishi wa habari Pemba(PPC) kwa kushirikiana na UN WOMEN

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.