Habari za Punde

KAMPUNI YA KK SECURITY YATAKIWA KUWALIPA WAFANYAKAZI WAKE MISHAHARA KWA WAKATI

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) Khamis Mwinyi Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana Kampuni ya Kenya Kazi Security  (KKS)  kutowalipa wafanyakazi wake mishahara kwa mujibu wa sheria (Kulia ) Katibu wa Chama cha Wafanyakazi  Kinachotoa  Huduma  kwa Jamii Ushauri Fedha na Viwanda Zanzibar Rihi Haji Ali na (Kushoto)  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi  Kinachotoa  Huduma  kwa Jamii Ushauri Fedha na Viwandani Zanzibar Mussa Yussuf.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi  Kinachotoa  Huduma  kwa Jamii Ushauri Fedha na Viwandani Zanzibar Mussa Yussuf akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari  kuhusu kutopatiwa wafanyakazi malipo yao (Kulia) Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) Khamis Mwinyi Mohamed (Kushoto) Mwanasheria wa Chama cha Wafanyakazi  Kinachotoa  Huduma  kwa Jamii Ushauri Fedha na Viwandani Zanzibar Ramadhani Juma Suleiman.

Wafanyakazi wa Chama cha Wafanyakazi  Kinachotoa  Huduma  kwa Jamii Ushauri Fedha na Viwandani Zanzibar wakimsilikiza Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) Khamis Mwinyi Mohamed (hayuop pichani).
                            Picha Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.
Na Mwashungi Tahir Maelezo Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi ZATUC Khamis Mwinyi Mohamed ameutaka Uongozi wa Kampuni ya Ulinzi ya Kenya Kazi (KK Security) kuwalipa mishahara wafanyakazi wa Kampuni hiyo kama sheria inavyotaka.
Wito huo ameutoa leo wakati akizungumza na Wanahabari ukumbi wa Elimu mbadala Rahaleo kuhusu tabia iliyozoeleka ya Kampuni hiyo kutolipa vyema stahiki za Wafanyakazi wao.
Amesema Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alitoa tamko rasmi la wafanyakazi kushughulikiwa maslahi yao kama ilivyo sheria na iwapo sheria hiyo haitofuatwa kampuni itakuwa imepinga amri ya Serikali na inafaa kuchukuliwa.
Hivyo amesema kampuni ya KK Security imepinga sheria iliyowekwa na kauli ya Rais kwa kutowalipa Kima cha Mishahara kilichowekwa na Serikali.
Aidha alisema kulimbikizwa kwa malipo ya wafanyakazi ni kuwanyima haki zao za msingi  na kuwataka waajiri wawalipe malimbikizo yao ikiwemo ya kufanya kzi kwa muda wa ziada kama ilivyoamuliwa na sheria ya  2017.
“Na natoa Rai kwa Mahkama ya kazi kuhakikisha kuwa kesi zinazopelekwa kuhusiana na ajira zinamalizika kwa haraka kwani kucheleweshwa kwa haki zao ndio kunyimwa haki hizo”alisema katibu huyo.
Katibu huyo pia aliwaonya wafanyakazi kukataa kudhalilishwa katika masuala ya kazi na kuwananishi pia kujiepushe kutumiwa na wajiri kuwadhalilisha wengine
Ametoa rai kwa Wafanyakazi kwa ujumla kuhakikisha kuwa linapotokea suala kuhatarishiwa maslahi yao kuripoti haraka katika chama cha wafanyakazi ili sheria ifate mkondo wake.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi kinachotoa huduma kwa jamii ushauri , fedha  na viwanda(ZAFICOWU) Mussa Yussuf  alisema hatua waliyofikia baina ya chama hicho na K K Security  ni kuhakikisha kuwa Wafanyakazi wanalipwa mishahara kama utaratibu wa Serikali unavyoelekeza.
Kwa upande wake Katibu wa chama hicho Rihi Haji  Ali  aliwataka waajiriwa  wote wafuate tamko la Waziri wa Kazi  Uwezeshaji  Wazee , Wanawake na Watoto Modeline Cyrus Castico aliyetaka Muajiri ambaye hajatoa mshahara kwa kipindi cha miezi miwili kuwalipa Mishahara kabla ya kupelekwa katika vyombo vya sheria.
Nao wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepaza sauti zao kuwa wanapata shida kwenye malipo yao ya mishahara kwa vile haitolewi kwa muda maalum wala siku maalum
Wamesema Kampuni hiyo ya KK Security inawasumbua sana kwenye malipo kwani hulipwa kidogo na huchukua muda mrefu kulipwa huo mshara mdogo hivyo wamesisitiza kupewa haki zeo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.