Wanafunzi
wa shule ya msingi Mzakwe ya Jijini Dodoma wakiwa mbele ya ukumbi wa Bunge leo
Jijini Dodoma.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola, akiwasilisha hotuba ya makadirio
ya mapato na matumizi ya wizara yake leo bungeni Jijini Dodoma.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola, akisisitiza jambo kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama (katikati) leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri Wizara ya Nishati, Mhe. Subira Mgalu, akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa
na serikali katika kuhakikisha kuwa gesi inawafikia wazalishaji katika viwanda vyote vilivyopo katika ukanda
unaopitiwa na bomba hilo kati ya Mtwara na Dar es Salaam kulingana na maombi ya
kuunganishiwa huduma hiyo.
Katibu
mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu,(wakwanza
kushoto) akifuatilia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi wakati Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola akiwasilisha hotuba hiyo leo
Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasilaino, Mhe. Atasashta Nditiye, akitoa ufafanuzi
kuhusu kuanza kwa zoezi usajili wa laini za simu kwa kwa kutumia alama za vidole
na kitambulisho cha taifa. Zoezi hilo linatarajiwa kuanza mwezi Mei na
kukamilika mwezi Disemba 2019.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, mhandisi Hammad Masauni, akisisitiza
kuhusu askari wa kikosi cha usalama barabarani kuzingatia sheria kanuni na
taratibu wanapotekeleza majukumu yao
leo Bungeni Jijini Dodoma.
(Picha
zote na Frank Mvungi- MAELEZO)
No comments:
Post a Comment