Mwenyekiti wa Bilal Muslim Africa Mohsin Abdallah (Shein) akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto ni Mkuu wa Maawal Sheikh Mohamed Hariri
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo |
Mratibu w Bilal Muslim Mission of Tanzania Sharriff akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa
Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na
Mratibu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Sharrif mara baada ya
kufanya uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Sehemu ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri Ummy wakati akizindua matibabu hayo
Wananchi kutoka maeneo
Sehemu ya wananchi wakisubiriwa kupata huduma ya matibabu wakati wa kambi hiyo
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye kambi hiyo ya macho
MAELFU ya Wakazi wa mji wa Tanga wamejitokeza kwenye kambi ya Matibabu
ya Macho inayoendelea kwenye shule ya shule ya Sekondari Maawal mjini
hapa chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission tanzania wakishirikiana na
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto chini ya Ufadhili wa
better Charity ya nchini Uingereza
Akizungumza wakati akizindua kambi hiyo ya matibabu ya Macho Waziri Ummy
alisema kuwa tatizo la ugonjwa wa macho nchini limekuwa kubwa ambapo
kila watanzania mia moja wanne wanakabiliwa na matatizo ya macho.
Alisema takwimu hizo zimefafanua kuwa katika idadi hiyo kila
mtanzania mmoja anakabiliwa na tatizo la upofu wa mamcho na watanzania
watatu wanakabiliwa na matatizo ya upungufu wa uoni wa kati na hali ya
juu tatizo ambalo limekuwa kubwa sana.
Aidha alisema kwa mujibu wa takwimu wizara ya afya katika kila
watanzania 100 mmoja ana tatizo la upofu huku kwa ikieleza kwa
watanzania 100 kati yao watatu wana matatizo ya upungufu wa kuona wa
kati na hali ya juu tatizo hilo ni kubwa kwa sababu kati ya watu 100 wa
nne wana matatizo ya macho.
Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy alitoa wito kwa watanzania kujiwekea
utaratibu wa kuhudhuria kwenye vituo vya Afya ili waweze kupata matibabu
pindi wanapoona kuwepo dalili za ugonjwa wa macho.
“Ukiona una tatizo la macho nenda kwenye vituo vya afya upate matibabu
haraka lakini niwaambie pia wana tanga na watanzania hakikisheni
mnachunguza afya ya macho na afya ya kinywa mara moja kila mwaka
“Alisema
Waziri huyo aliwataka watanzania kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa
hasa vyenye vitamin ikiwemo kuhakikisha wanakula mbogamboga huku
akiwataka kuacha dawa kwenye macho bila kuandikiwa na daktari kwa sababu
inaweza kupelekea kuharibu macho yao
Awali akizungumza katika halfa hiyo Mwenyekiti wa Bilal Muslim Afrika
Mohsin Abdallah (Shein) alimshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa
kuhakikisha huduma za afya nchini zinaimarika kwenye maeneo mbalimbali
na kuondosha changamoto zilizopokuwepo awali.
“Namshukuru Rais Magufuli miaka yote tumefanya kazi tunatumia hospitali
za serikali huduma zilikuwepo lakini hazikuwa kama ilivyo sasa lakini
leo serikali ya awamu ya tano hospitali zimekuwa na vifaa muhimu kwenye
hospitali”Alisema
Aidha alisema wao kama bilal Muslim wamekuwa wakienda kwenye maeneo
ambayo yana matukio makubwa lakini kutokana na ombi la Waziri Ummy
tumeona kuja hapa kumuunga mkono pia tunashukuru mwamko umekuwa mkubwa
sana,
No comments:
Post a Comment