Habari za Punde

Mkuu wa Takwimu za bei atoa Faharisi za Bei kwa Zanzibar

 Mkuu wa Takwimu za Bei katika Ofisi kuu ya Takwimu Zanzibar Khamis Abdul-rahman Msham akitoa maelezo ya Takwimu za Bei ambapo imeonekana kupanda kutoka asilimia 2.6 kwa mwaka uliomalizia February 2019 hadi asilimia 2.8 March 2019 hafla iliofanyika Ofisi kuu ya Takwimu Mazizini Zanzibar.
 Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Dk,Suleiman Msaraka akitoa ufafanuzi baadhi ya maswali yalioulizwa katika hafla ya utoaji wa Takwimu za Bei  Ofisi kuu ya Takwimu Mazizini Zanzibar. 
 Mkuu wa Idara ya Takwimu za Kiuchumi Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Abdul Ramadhan Abeid akijibu baadhi ya maswali yalioulizwa   katika hafla ya utoaji wa Takwimu za Bei  Ofisi kuu ya Takwimu Mazizini Zanzibar. 
Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi Benki kuu Tawi la Zanzibar Deogratias Macha akijibu maswali yalioulizwa   katika hafla ya utoaji wa Takwimu za Bei  Ofisi kuu ya Takwimu Mazizini Zanzibar. 

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.