Habari za Punde

Halmashauri ya Magharibi B Unguja Wapokea Msaada wa Madari ya Kuzolea Taka taka.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Magharib B Unguja Ndg.Ali Abdalla Natepe akikabidhiwa mfano wa Fungo za Magari kutoka kwa Afisa Mauzo wa kampuni ya GF Trucks Ndg.Filbert Peter wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya kampuni hiyo, Halmashauri ya Magharibi B Unguja imekabidhiwa magari kwa ajili ya kubebea taka, katiika Halmashauri hiyo kushoto akishuhudia Meya wa Halmashauri ya Manispa ya Magharibi Unguja Mhe. Maabad Ali Maulid.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Magharib B,Alli Abdalla Natepe akipokea zawadi ya tuzo kutoka kwa AfisaMauzo wa kampuni ya GF Trucks ,Filbert Peter wakati wahaflaya kukabidhi Magari na mitambo ya kubebea takataka katika halmashauri hiyo Mjin Zanziba.Katikati ni Mweya yamji huo Maabad AlI Maulid




Na mwandishi wetu
Wakati mvua za masika zikiendelea katika maeneo mingi ya Tanznaia, Manispaa ya wilaya ya magharib B  Unguja imejipanga kikamilifu kuhakikisha hali ya usafi wa mazingira unaimarika.
Kuimarika kwa usafi huo kunatokana na manunuzi ya vifaa vipya vya usafi pamoja na magari na mtambo maalumu wa kukusanyia taka ambapo jumla ya shilingi milioni mia nne zimetuma katika ununuzi wa vifaa hivyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hivyo   Mkurugenzi wa manispaa hio Ali Abdalla Natepe alisema ununuzi  wa vifaa hivyo utaongeza ufanisi mkubwa katika ufanyaji wao wa kazi za kila siku.
Baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa ni toroli,ndoo za kuhifadhia taka,vifaa maalumu vya kujikinga na uchafu(glovers) pamoja na magari na mtambo wa kukusanyia taka.
AlisemaUnunuzi wa vifaa hivyo utasaidia kupunguza tatizo la mludikano wa taka ambalo lilikua sugu katika halmashauri hio kutokana na uwepo wa vifaa duni vya kufanyia  kazi hali ambayo iloiopelekea maeneo mengi kuwa na mlundikanowa taka taka.
Alieleza kuwa kuwepo  kwa vifaa hivyo vipya kutawawezesha kufanya kazi katika majaa mbali mbali yaliorasmi na yasiorasmi na kwamba kutawasadia pia wananchi kuepuka na maradhi.
Aidha alisema licha ya kukabiliwa na chanagamoto hizo hazikuwafanya warudi nyuma badala yake waliendelea kutekeleza wajibu wao wakati mwengine kwa kukodi gari maalumu.
Mwakilishi wa kampuni ya  GF Track afisa mauzo Filbert Peter alisema wataendelea kutoa mashirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuhakikisha utendaji kazi unaimarika.
Hata hivyo kampuni hio imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa mafunzo kwa madereva na mafunzi kw alengo la kuongeza ufanisi kwenye vifaa hivyo vipya.
Aidha alisema magari hayo mawili pamoja na kijiko cha kubebea taka ni ya kisasa na yana uwezo mkubwa wa kufanya kazi mbali mbali kinyume na iliokusudiwa ya kuzolea taka pekee ikiwemo kusaidia katika shughuli mbali mbali za kiuchumi wa Taifa.
Kwa upande wake mstahiki mea wilaya ya magharib B Unguja Maabad Ali Maulid alisema ipo haja watendaji wa manispaa hio kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa pamoja na kuvitunza vifaa hivyo vipya na ili viweze kudumu kwa miaka mingi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.