Habari za Punde

Wanafunzi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mwaka Huu Wanatarajiwa Kuleta Mafanikio Makubwa Katika Ufauli wa Mitihani yao ya Taifa Kidatu cha Nne na Sita.

Na Mwashungi Tahir       Maelezo     9-4-2019.
Serikali itaendelea kuzidisha juhudi kwenye sekta ya  Elimu na  kuhakikisha wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Taifa kwa kidato cha sita na cha nne katika skuli zote za Serikali na Binafsi zinafanya vizuri na kuongezeka ufaulu.
Hayo ameyasema Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud huko katika ukumbi wa sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kidato cha sita ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Alisema katika Mkoa wa Mjini Magharibi mwaka huu wanafunzi hao wanatarajiwa kuleta mafanikio makubwa katika upatikanaji wa ufaulu wa mitihani yao kwa vile fursa nyingi zishatolewa ili wapasi kwa wingi ikiwemo vitabu vya masuala na majibu.
“Natarajia katika mwaka huu ufaulu utaongezeka hasa ukuzingatia rai nyingi zimetolewa ili wanafunzi washike nafasi zinazotakiwa ili kuunga’risha Mkoa huo kwa kubadilika kujibu masuala kama inavyotakiwa na Baraza la Mitihani” alisema Mkuu wa Mkoa huyo.
Ayoub aliwataka wazazi , walezi wa wanafunzi pamoja na walimu kukaa nao wanafunzi hao nakuwapa mashirikiyano ambayo yataweza kuwaletea ufaulu kwa hali ya juu na kuwa watulivu katika kambi kwa kuwapelekea chakula cha kutosha kwa siku zote watazokuwepo kambi.
Aidha amesema kamati ya maendeleo ya elimu imefanya jitihada kwa skuli zote zilokuwemo nyuma kwa matokeo mabaya na kuweza kuzisogeza na kutarajia mwaka huu kuleta mabadiliko ya ufaulu kwa wingi.
Pia aliwaahidi walimu watakaopasisha “A” watazawadiwa sh laki moja na mwanafunzi atakapata alama ya A atazawadiwa laki mbili na Laptop hii yote lengo lake kuwaweka vizuri wanafunzi katika kushughulikia masomo yao na kuwambia ahadi za Rais zipo vile vile.
Hivyo Ayoub aliwaomba wanafunzi kuacha mambo ya anasa ikiwemo simu  na kujipanga kwenye masomo ili waweze kufikia ndoto zao za maendeleo na kujiweka vizuri kimaisha kwani ulimwengu wanaokwenda nao ni wa elimu na ndio tutapata wataalamu wazuti katika utendaji wa kazi.
Akitoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kujitokeza kwa wingi katika kusaidia vyakula kwa wanafunzi watakao kuwa kwenye kambi kwani wakitoa kwa ajili ya kupatikana elimu ndio wanaimarisha Mkoa wa Mjini Magharibi .
Nae Mkurugenzi  wa Global kwenye masuala ya elimu Abdul malik   S. Mollel aliwataka wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kidato cha sita kuzidisha juhudi ili kufikia matarajio waliyoyakusudia.
Aliwapa rai jinsi ya kuchukuwa masomo na kuweza kufaulu na hapo baadae kuweza kuingia kwenye vyuo na kutoka hapo ndoto zao kutimia ikiwa daktari, injiniiya, biashara na mambo mengine na kuwahakikishia fursa zipo iwapo watafaulu vizuri.
Kwa upande wa wazazi na walezi walimu na  wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kuwasaidia ulezi mzito kwani wengi kutokana na hali zao kuwa dhaifu walishindwa watoto wao kuwaweka kaqmbi kutoana na kushindwa kutoa huduma zinazotakiwa .
“Tunamshukuru mkuu huyo kwa kutusaidia suala zima la huduma za kukaa kambi wengi tulishindwa kulipia gharama zake hivyo tunamuomba mungu amzidishie kheri na ampe wepesi katika maisha yake ya kila siku”, walisema wazazi hao.
Vile vile wanafunzi nao walitoa shukurani zao kwa  Serikali pamoja na Mkuu wa Mkoa na kuahidi watajitahidi badala ya A 99 mwaka huu zitapindukia zaidi katika mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.