Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Ajumuika Katika Futari Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba.

Wawakilishi wa Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba wakijumuika pamoja katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa  Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kufanyika katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdullah akitoa salamu kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya Futari ya pamoja hapo Wawi.
Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdullah akitoa salamu kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya Futari ya pamoja hapo Wawi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibare Mhe Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Wananchi mbali mbali waliowawakilisha wenzao wa Mikoa Miwili ya Pemba baada ya Futari ya pamoja hapo Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibare Mhe Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Wananchi mbali mbali waliowawakilisha wenzao wa Mikoa Miwili ya Pemba baada ya Futari ya pamoja hapo Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibare Mhe Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Wananchi mbali mbali waliowawakilisha wenzao wa Mikoa Miwili ya Pemba baada ya Futari ya pamoja hapo Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis.OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesisitiza umuhimu wa Jamii kuendeleza kuitunza Amani na kudumisha Umoja miongoni mwao inayotoa fursa kwao kufanya shughuli zao za kimaisha bila ya wasi wasi wakati mataifa mengine imekuwa adimu kuipata kutokana na uhasama usiokwisha.
Alisema Taifa limeweza kupiga hatua kubwa katika kuimarisha Uchumi na maendeleo ya Wananchi wake kulikosababishwa na uwepo wa Amani ambayo haikuja bure bali ni jitihada zilizochukuliwa na Wananchi wenyewe chini ya usimamizi wa Viongozi wao wa Kitaifa.
Balozi Seif alitoa sisitizo hilo katika salamu za ukumbusho zilizotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pembe Mh. Hemed Suleiman Abdullah mara baada ya Futari ya pamoja iliyowajumuisha Wawakilishi wa Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba iliyofanyika  hapo katika Ukumbi wa Mikutano  wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Alisema wapo baadhi ya Binaadamu wa Mataifa tofauti Duniani ambao kipindi hichi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wanafunga na kufutari katika kambi za Wakimbizi kufuatia Mataifa yao kuyayuka kwa Amani iliyokosekana kutokana na vurugu za kuhatarisha Maisha yao zilizopelekea kuyakimbia makaazi yao halisi.
“ Amani lazima iendelee kuwepo Nchini kwa vile hakuna jaribio wala mbadala kwenye suala hilo muhimu katika maisha na ustawi wa kila siku wa Mawnaadamu”. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kwa vile Jamii imekuwa huru na shuwari katika harakati zao za Kimaisha ndani ya Amani iliyopo aliwahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kudumisha suala la Ibada kwa vile ni wajibu kwao kufanya hivyo.
Alieleza kuwa Mwanaadamu uwepo wake Ulimwenguni kaumbiwa kwa kazi moja tu ya kumuabubu Mola wake aliyemuumba Subuhanahu wataala. Hivyo Mja huyo analazimika kujiwekea malengo imara katika Maisha yake ya kudumu atakaporejea katika himaya ya Mola wake.
Balozi Seif pamoja na mambo mengine amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu kuzidisha Ibada zao ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao umeshushwa Kitabu Kitakatifu cha Quran Karim pamoja na Usiku wenye cheo wa Lailatul Qadri.
Akikariri baadhi ya Aya za Kitabu hicho Balozi Seif alisema Suratul Baqra katika aya ya 23 imeweka wazi ikiwaeleza Waumini hao kufaradhishiwa Ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukiwa miongoni mwa Nguzo Tano anazowajibika kila Muumini wa Dini ya Kiislamu kuzitekeleza.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdullal alitumia fursa hiyo kwa niaba ya Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba kuwapa pole Wananchi wenzao wa Unguja waliopatwa na Maafa kufuatia Mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha Nchini.
Mh. Hemed alisema Wananchi wa Pemba wanaungana na wenzao wa Unguja waliopatwa na mtihani huo katika kipindi hichi kigumu cha ukosefu wa Makaazi yao ya kudumu baada ya nyumba zao kujaa maji.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Viongozi wa Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba mara baada ya Futari hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa alisema Balozi Seif ni Kiongozi wa Watu anayeonyesha mfano wa kuwa karibu na Wananchi anaowaongoza muda wote.
Mzee Mberwa alielezea faraja yake kutokana na mvua za masika za mwaka huu zinazoendelea kunyesha zimeweza kuongeza baraka hasa Kisiwani Pemba ya mahitaji ya vyakula mbali mbali vilivyopelekea kupatikana kwa futari za kila aina.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.