Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Awasili Kisiwani Pemba Kwa Ziara Maalum ya Kujumuika na Wananchi wa Mikoa Miwili Katika Futari Aliowaandalia

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba akiwa katika ziara Maalum ya kujumuika na Wananchi wa Kisiwani Pemba wa Mikoa miwili katika futari aliyowaandali, inayotarajiwa kufanyika leo jioni , kushoto Mshauri wa Rais Afisi ya Rais Pemba Dr. Maua Daftari.   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkuu wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Kisiwani Pemba akiwa katika ziara Maalum ya kujumuika na Wananchi wa Mikoa Miwili ya Pemba katika futari maalum inayotarajiwa kufanyika leo jioni. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa Kisiwani Pemba alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Kisiwani Pemba,alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Mkewe Mama Mwanamwema Shein na kulia Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman, wakielekea katika chumba cha mapumziko baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege Chakechake Pemba leo mchana kwa ziara maalum.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.