Habari za Punde

Savana International Kukabidhi nguo Kwa Watoto Wenye Mazingira Magumu

Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar 07.05. 2019.
Kampuni ya Savana International inayojishughulisha na uuzaji wa nguo nchini imetoa msaada wa Nguo na Vitambaa wenye thamani ya TShilingi milioni 80 kwa Watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwafariji katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hafla ya kukabidhi Msaada huo ilifanyika Msikiti wa Fysabilillah Aman mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi wa Kampuni hiyo, Walezi pamoja na watoto hao.
Akikabidhi msaada huo Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Ramadhani Shaame Ali amewataka watu wenye uwezo kujitokeza kwa wingi kusaidia watoto wenye mahitaji maalum hasa katika katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.
“Nawaomba watu wenye uwezo kujitokeza kwa wingi wenye uwezo wawasaideie watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kuwasidia na wao wajisikie kama wanaishi na waze wao”, alisema Afisa huyo.
Amesema iwapo Watu wenye uwezo watajitokeza kuisadia jamii iliyo na mazingira magumu watapa malipo kwa Mwenyezi Mungu duniani na akhera.
Afisa Ramadhan amefahamisha kuwa wapo baadhi ya watoto yatima wanaokosa msaada na mahitaji muhimu ikiwemo nguo, kusoma na huduma nyengine na hivyo kuwapelekea unyonge katika maisha yao.
Amesema hali hiyo huwakosesha furaha katika maisha yao na kuwaomba watu wenye uwezo kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao.
Wakitoa shukran zao kwa msaada huo Walezi wa watoto hao wamesema wamefarijika sana kwa kile walichopatiwa ambacho kitawapa faraja wao na watoto wao.
Wamesema hali ya maisha imekuwa ngumu na hivyo kushindwa kuzihudumia vyema familia zao kutokana na uwezo mdogo wa kipato waliokuwa nao.
Wametoa wito kwa Watu wengine wenye uwezo kujitokeze kwa wingi kusaidia watoto hao kwani kufanya hivyo kutapa fadhila duniani na Akhera.
Jumla ya milioni Thamanini zimegharimu mzigo wa Nguo na Vitaa hivyo kutoka nchini Canada ambapo Watoto wa umri wa miaka sita hadi 17 hupatiwa kila mwaka maeneo ya Mjini na Vijijini ili kuwafariji kipindi cha Ramadhani na Siku kuu ya Eid.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.