Habari za Punde

Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Wajumuika katika Futari ya Pamoja

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Tatu kutoka Kushoto akifuatiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Zubeir Ali Maulid na Mkuu wa Mkoa Mjini Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud wakijumuika na Watendaji wa Ofisi yake katika Futari ya pamoja.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wa Pili kutoka Kulia akijumuika pamoja na Watendaji wa Ofisi hiyo katika Futari ya pamoja iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi wa Kitaifa na baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi za Serikali akipata Futari kwenye Hafla hiyo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa shukrani kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa washiriki wa Futari ya pamoja  hapo Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Balozi Seif Kushoto akiagana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud huku Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Zubeif Ali Maulid pamoja na Waziri Mohamed Aboud wakifurahia tendo hilo.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Waumini wa dini ya Kiislamu Nchini wanaendelea na Ibara yao ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao ni nguzo ya Nne ya Uislamu wakiwa ndani ya Kumi la Kwanza la Rehma.
Ibada ya funga ya Mwezi huo huwafanya Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuwa na Taqwa, Mapenzi na Ucha Mungu unaowafanya kuelekeza zaidi nguvu zao katika Kumcha Mwenyezi Muungu Subuhana hu wa Taala.
Moja kati ya jambo kubwa na zito ambalo Waumini hao hulitekeleza ndani ya Mwezi wa Ramadhani ni kufutari, kunywa na kulal pamoja kitendo kinacholeta faraja na mapenzi ya Dini miongoni Mwao.
Harakati za utaratibu huo zimeanza kwa makundi mbali mbali hapa Nchini likianza na lile la Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar chini ya Kiongozi wao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walipojumuika katika Futari ya pamoja iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Akitoa Shukrani kwa Niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed aliishukuru na kuipongeza  Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwa umahiri wake wa kuendelea kuishauri Ofisi hiyo.
Mh. Aboud alisema umahiri wa Kamati hiyo katika ushauri wake wa masuala mbali mbali yanayoihusu Ofisi hiyo imewawezesha Viongozi na Watendaji wake kutekeleza majukumu yao kwa urahisi zaidi yakiwemo Makadirio ya Mapato na Matumazi yake kwa Miaka tofauti.
Futari hiyo mbali ya kutoa nafasi ya kunywa na kula pamoja lakini pia iliwapa fursa nyengine Watumishi wa Ofisi hiyo kutafakari Kitendo cha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwenye Baraza hilo lililoanza kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/2020.
Futari hiyo ya pamoja ilijumuisha Viongozi Wakuu, Maafisa Watendaji na baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi zote  zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.