Habari za Punde

DC TANGA AWATAKA MADIWANI,WENYEVITI WA MITAA KUPIGA VITA BIASHARA ZA MAGENDO KWENYE MAENEO YAO KWANI VINATIA DOA-DC MWILAPWA

MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifungua semina ya wenyeviti wa Mitaa na Madiwani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Tanga 
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim akizungumza wakati wa semina hiyo
Mwakilishi wa Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarura ambaye ni Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA Tanga
Meneja Msaidizi Idara ya Forodha Edward Ndupa akizungumza katika semina hiyo
Ofisa wa Elimu kwa Mlipakodi Mkoa wa Tanga Salim Bakari akizungumza wakati wa semina hiyo
MKUU wa Kitengo cha  Kodi za Majengo TRA Mkoa wa Tanga John Minja akieleza umuhimu wa ulipwaji wa kodi hizo wakati wa semina hiyo
NAIBU Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu akizungumzaa
 Mwenyeviti wa Serikali Mitaa kwenye Jiji la Tanga Maimuna Ramadhani kutoka Mtaa wa Mabawa Mikanjuni A akiuliza swali wakati wa semina hiyo
 Diwani wa Kata ya Majengo (CUF)
 Diwani wa Kata ya Msambweni Jijini Tanga (CUF) Abdurahamani Hassani katikati akiwa na madiwani wengine kwenye semina hiyo
 Sehemu ya Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wakifuatilia semina hiyo

 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka wenyeviti wa mitaa na madiwani kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kupiga vita biashara za magendo ikiwemo kuwafichua wanaohusika kwenye maeneo yao kwani vinawatia doa.

Mwilapwa aliyasema hayo leo wakati akizungumza na madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa katika semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Tanga.

Alisema kwamba wilaya ya Tanga kuna tatizo kubwa hata wakati fulani Rais Dkt John Magufuli alikwisha kutaja kwani miongoni mwa wilaya zenye vipenyo vingi vya uingizaji bidhaa bila kufuata utaratibu kupitia Bandari rasmi.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kwenye semina hiyo alisema kwamba hivi sasa wamejipanga imara kuweza kuhakikisha mianya yote haipitisha bidhaa kwa njia zisizo rasmi kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali.

Aidha pia aliwataka viongozi hao kushirikiana na watu mbalimbali ikiwemo kuhakikisha biashara na shughuli zinazoendeshwa ndani ya wilaya zinakwenda kwa utaratibu unaokubalika.

“Lakini suala la biashara ya magendo tumekuwa tukiipigia kelele kila wakati tumekuwa na tabia ya kuingiza bidhaa kwa njia za panya tabia hii inatukera tumekuwa tukipambana nalo na tunaamini litakwisha kabisa”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema anaamini semina hiyo itawapa uelewa mkubwa ambao utakuwa chachu kwenye maeneo yao kwa sababu ni wanasiasa wana ushawishi kwa jamii watumie njia mbalimbali kuweza kuwapa elimu jamii itasaidia kupunguza na hatimaye kumaliza magendo.

“Lakini pia wataalamu na wanasiasa tukishikamana kwa pamoja tunaweza kumaliza tatizo la magendo huku akiwataka viongozi wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo kwani wakikamatwa wataishi kwenye mikono ya kisheria”Alisema

Awali akizungumza katika semina hiyo Mwakilishi wa Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarura ambaye ni Meneja Msaidizi Upande wa Madeni TRA Tanga alisema wameitisha kikao hicho cha madiwani na wenyeviti ili kuwaelimisha masuala mbalimbali kuhusu kodi kwani wao ni nguzo kuu ya wananchi ili waweze kuipeleka elimu hiyo.

Alisema pia semina hiyo imelenga kwenye umuhimu wa kodi,Masuala ya EFD Mashine ,kutoa na kudai risiti,Elimu ya umuhimu wa kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ada za mabango kwa sababu wapo karibu na wananchi wakifikisha huko inaweza kuwa chachu ya kuongeza mapato.

Hata hivyo alisema suala la magendo sio mazuri kwa sababu yanaikoseka mapato serikali hivyo wanaimani watafanikiwa kuliondosha.

Naye kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msambweni (CUF) Abdurhamani Hassani alisema baada ya elimu hiyo wamejifunza mambo mengi hasa suala la magendo jambo ambalo linaathiri ukusanyaji wa mapato.

Alisema yapo magendo yanafanyika kutokana na kuwepo kwa uelewa mdogo kwa wale wafanyabiashara kwa sababu ukitazama viwango cha kodi vinalipika watajiahidi kwenye kueilimisha jamii kwa sababu kodi sio jambo la hiari bali ni lazima.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.