Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasalimia na kutowa Mkono wa Eid Fitry, kwa Wazee wa Nyumba ya Wazee Sebleni Zanzibar, alipofika kuwatembelea leo akiwa na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleima Iddi.
WATOTO wanaoishi katika nyumba za kulelea watoto katika kijiji
cha SOS na Mazizini, Mkoa Mjini Magharibi Unguja, wametakiwa kuwa makini na
wasikivu katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Eid el Fitri ili kuepukana
na vitendo hatarishi.
Indhari
hiyo imetolewa na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na watoto
Moudline Castico, kwa wakati tofauti alipokuwa akitowa shukrani kwa Mke wa Rais
wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,
Mama Asha Suleiman Idd, baada ya kukamilika hafla ya utowaji wa zawadi za
Sikukuu kwa wazee wanaotunzwa na Serikali, nyumba za wazee Welezo, Sebleni pamoja na watoto wanaolelewa
katika vituo vya SOS na Mazizizni.
Aliwataka
watoto hao kuwa wasikivu wakati wanapokwenda na kurudi katika viwanja vya
sikukuu pamoja na kufuata maelekezo ya wakubwa zao, ili kuepukana na matukio
mbali mbali yanayoweza kuhatarisha usalama wao.
Alisema
ni vyema kuwa pamoja wakati wote wa sikukuu na kufuata malekezo yanayotolewa.
Aidha,
Waziri Castico aliwapongeza viongozi hao kwa kuendeleza utamaduni wa
kuwatembele na kuwapa zawadi wazee na watoto hao kila nyakati za sikukuu
zinapofika.
Alieleza
kuwa hatua hiyo inaendeleza imani na upendo kwa wazee na watoto hao.
Nae,
Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii Zanzibar, Wahida Maabad aliwashukuru viongozi hao
kwa kuendeleza utamaduni wa kuwapatia futani na zawadi za sikukuu wazee na
watoto hao
Alisema
hatua hiyo inawapa faraja na kuamini kuwa ni sehemu ya jamii ambayo
inathaminiwa.
Katika
hafla hiyo jumla ya wazee 37 kutoka nyumba za kutunzia wazee Welezo
walizawadiwa, sambamba na wazee 35 wanaoishi katika nyumba za wazee Sebleni.
Aidha,
watoto 35 wanaoishi katika nyumba ya
kulelea watoto Mazizini pamoja na watoto 180 wanaoishi atika Kijiji cha kulelea
watoto SOS walizawadiwa.
Katika
mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, kwa nyakati tofauti viongozi hao walipata
fursa ya kufutari pamoja na watoto wa vituo vya SOS na Mazizini, ikiwa ni utaratibu
wao wa kila mwaka.
Abdi Shamna, Ikulu
Zanzibar
Postal
Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822
E-mail: abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment