Habari za Punde

Seif Kombo Aibuka Mshindi Katika Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Shikisho la Michezo Zanzibar ZFF, Uliofanyika Jana

Rais Mpya wa Shirikisho la Michezo Zanzibar Ndg Seif Kombo, aibuka kidedea katika Uchaguzi Mkuu wa ZFF uliofanyika jana katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani Zanzibar, na Kikiongoza Chama hicho Baada ya kupitishwa kwa Katiba Mpya.  
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo Zanzibar ZFF Ndg Salum Ubwa, amishiunda Nafasi hiyo katika uchaguzi Mkuu uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani Zanzibar.  

Na Hawa Ally,. ZAnzibar
SEIF Kombo ameibuka kidedea kwa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF kwa silimia 57. 85 katika uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo ulifanyika hapo jana. 

Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF Fadhir Ramadhani amemtangaza mgombea Seif Kombo Pandu kuwa Rais wa Shirikisho hilo baada ya kuibuka mshindi kwa  kupata kura 16 sawa na asilimia 57 kati ya kura 28  za wajumbe wote waliopiga. 

Mgombea huyo ambae aliwamwaga wagombea wenzake Ame Abdalla Dunia ambae alipata kura 5 sawa na asilimia 17.85%, Mgombea mwingine ni Khamis Abdalla Said ambae alipata kura 7 sawa na asilimia 25.00%

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Shirikisho hilo Mwenyekiti Alimtangaza Salum Ubwa kuwa makamu kwa kupata kura 25 sawa na asilimia 89.2, akimbwaga aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo Khamis Shaali aliyepata kura 3 sawa na asilimia 10.7.

Aidha mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi aliwatangaza wajumbe wa kamati tendaji kwa ngazi ya Mikoa ambapo kwa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, Suleiman Haji aliibuka kidedea kwa kupata kura 18 sawa na asilimia 64.21 akimbwaga Faina Idarous aliyepata kura 10 sawa na asilimia 35.7

Kwa upande wa Mkoa wa Kusini Unguja mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi aliwatangaza Salim Ali kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji kwa kupata kura za ndio 27  katika ya kura 28 sawa na asilimia 96.4 huku kura.

Wakati katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Seif Bausi aliibuka kidedea kwa kupata kura 19 sawa na asilimia 67.85, akimpiku Rashid Tamimu aliyepata kura 9 sawa na asilimia 32.14

Aidha Kwa Upande wa Mikoa ya Pemba Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi imemtangaza Omar Awadhi kuwa mshindi wa nafasi hiyo Kwa mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kupata kura zote 28 sawa na asilimia 100. 

Wakati katika mkoa wa Kusini Pemba Seif Mohmmed ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura zote 28 sawa na asilimia 100.

Awali akifungua mkutano huo mkuu Katibu mkuu wa Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo Omar King aliwataka wagombea watakaochaguliwa wahakikishe wanasimamia vyema soka la Zanzibar kwa kuiba vipaji katika mikoa na Wilaya maeneo ya vijijini badala ya kuangalia maeneo ya mjini Pekee. 

Alisema ni wakati umefika kupitia vyama vya mikoa kuhakikisha mpira wa Zanzibar unakuwa kuanzia katika mikoa yao na hadi wilaya zote za Zanzibar kama ilivyokuwa katika miaka ya 80

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.