Habari za Punde

Balozi Seif akagua eneo la maalum kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za SMZ jijini Dodoma

 Muonekano wa eneo la Mtama lililoanza harakati wa Ujenzi wa Majengo ya Ofisi ndani ya Mji Mpya wa Dodoma baada ya Serikali kuamua shgughuli za Serikali zihamie kwenye Mji huo uliopo kati kati ya Tanzania.
 Msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ukiwa njiani kuelekea eneo lililotengwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba kujenga Majengo yake ndani ya Mji Mpya Jijini Dodoma.
 Katibu wa Kuhamia Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nd. Meshack Bandawa wa Pili kutoka Kushoto akimuonyesha Ramani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  wa Pili kutoka Kulia jisi Mji Mpya wa Dodoma utakavyokuwa baada ya kujengwa.
Kulia ya Nd.Meshack ni Afisa Ramani wa Manispaa ya Jiji la Dodoma Nd. Willia n a kushoto ya Nd. Meshack ni Mkurugenzi Uratibu wa SMT  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Khalid Bakar Amrani.
Kulia ya Balozi Seif  ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Nd. Joseph Edward Moringe na Waziri wa Baisha na Viwanda Zanzibar Balozi Amina Salum Ali
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Nd. Joseph Edward Moringe Kushoto akimkaguza Balozi Seif  sehemu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayotarajiwa Kujengwa Ofisi zake ndani ya eneo la Mtama Mjini Dodoma.
Katibu wa Kikosi Kazi cha kusimamia kuhamia Dodoma Nd. Meshack Kushoto akimounyesha Balozi Seif na Balozi Amina Salum Mlima uliopo kati kati ya Mji Mpya wa Dodoma utaowekewa alama Maalum ikitoa ishara ya kumtambulisha Mtu ye yote anayesafiri kuelewa kwamba anaingia  Ndani ya Mji Mpya wa Dodoma.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, Dodoma
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kuipatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar eneo Maalum kwa ajili ya Ujenzi wa  Ofisi zake Ndani ya Mji Mpya wa Makao Makuu ya Nchi Mjini Dodoma.
Alisema kitendo hicho kilichofanywa na SMT  kitabakia kuwa Historia ya kuendelea kuimarika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  uliozaa Jamuhuri ya Muungano wa  Tanzania uliodumu karibu Miaka  55 sasa unaozifanya Serikali zote mbili kufanya Kazi kwa ukaribu zaidi.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa shukrani hizo wakati alipofanya ziara Maalum ya kutembelea eneo lililokabidhiwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Kujenga Ofisi zake katika eneo la Mji Mpya wa Mahoma Makulu  Kilomita takriban 17 nje kidogo ya Jiji la  Dodoma.
Alisema wakati SMZ inatafakari namna ya kuanza Ujenzi wa Ofisi zake katika Bajeti ya Mwaka ujao kuna haja kwa Taasisi zilizokuwa tayari kuanza hatua za awali za Mradi huo si vibaya zikaiga Ujenzi wa Taasisi zilizoendelea katika Upangaji wa Miji Mipya ya kisasa.
Balozi Seif alisema wakati umefika kwa Wataalamu wa Kizalendo wa Ujenzi na Mipango Miji kuepuka makosa yaliyofanywa na Wakoloni wakati wa Ujenzi wa Miji ambayo kwa sasa imekuwa ya asili ikishindwa kutoa huduma zinazostahiki kwa baadhi ya wakati kutokana na kukosekana kwa utaratibu wa Kitaalamu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikipongeza Kikosi Kazi cha kuhamia Dodoma chenye Wajumbe kutoka pande zote Mbili za Tanzania Bara na Zanzibar kwa kazi kubwa wanayoendelea kuisimamia katika kusarifu Ujenzi wa Mji Mpya Jijini Dodoma.
Balozi Seif  aliuomba Uongozi wa Kikosi Kazi hicho kutembelea Zanzibar na kuonana na Viongozi pamoja na Wananchi kwa lengo la kutoa Taaluma ya uwelewa wa jinsi gani Mji Mpya wa Jiji la Dodoma unavyotarajiwa kuwa.
Mapema Katibu wa Kuhamia Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nd. Meshack Bandawa alisema Kikosi Kazi chake kimeanza kuwajibika  mara tu baada ya Rais wa  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kutangaza shughuli za Serikali zihamie Dodoma Mnamo Tarehe 25 Julai Mwaka 2016.
Nd. Meshack alisema Kikao Kazi hicho kwa kushirikiana na Wataalamu wa Sekta mbali mbali za Umma kilianza na hatua za kupima eneo la Mji Mpya linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa Hekta Mia 664 kazi iliyokwenda sambamba na utaratibu wa kulipa Fidia kwa Wananchi na Taasisi zilizokuwemo ndani ya eneo hilo.
Alisema hatua hiyo iliwawezesha kuanza upimaji wa Maeneo ya Taasisi   zilizopewa maeneo yenye ukubwa wa Hekta 2.5 zikiwemo Wizara za Serikali zilizokwishaanza kujenga, Ofisi za Kibalozi, Majengo ya Biashara, maeneo ya Bustan, Michezo pamoja na Burdani.
Nd. Meshack alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pekee ilipatiwa Ekari 30 kama ilivyoomba maombi yaliyozingatiwa katika hatua zote za maamuzi.
Alifahamisha kwamba  Majengo 23 ya Wizara 23 za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tayari  yameshajengwa chini ya Wataalamu na Wahandisi wa Taasisi za Kizalendo hapa Nchini, ujenzi uliokwenda sambamba na utayarishaji wa Miundombinu ya huduma za Umeme na Maji safi na salama.
Mkuu huyo wa Kikosi Kazi cha kusimamia Mradi wa kuhamia Dodoma alieleza kwamba Awamu ya Pili ya Ujenzi wa Majengo mbali mbali ndani ya Mji Mpya wa Dodoma itahusisha Ujenzi wa Majengo marefu ya Ghorofa pamoja na Bara bara za Lami.
Nd. Meshack alisema Majengo hayo marefu yatajengwa  kwa kuzingatia  Ushauri uliokidhi Kitaalamu  kufuatia Takwimu zilizofanywa na Wataalamu  kuanzia Mwaka 1966 hadi 2017 juu ya mazingira ya Mkoa wa Dodoma unaopata Mitetemeko ya Ardhi ambayo muda wote bado haijaleta athari yoyote.
Kwa upande wake Afisa  wa Upimaji  na Mipango Miji wa Manispaa ya Jiji la Dodoma Ndugu William Uhayo alisema Ramani kamili ya ujenzi wa Nyumba za Viongozi pamoja na mambo mengine yanayoupamba Mji  imekamilika.
Nd. William alisema Ramani hiyo inaonyesha namna Mji Mpya wa Dodoma utakavyokuwa na Bara bara kubwa za kisasa zitakazotiwa Lami yenye urefu wa Kilimo Mita 110 na kuuzunguuka  Mji wote.
Alisema Tangi kubwa la kusambazia huduma za Maji ndani ya Mji Mpya limeshajengwa likiwa na uwezo wa kuhifadhi maji Qubic Mita 1,000 ambapo katika hatua ya baadae Minara Minne  itajengwa ili kurahisisha huduma za Mawasiliano ndani ya Mji huo.
Alifahamisha kwamba mpango wa uimarishaji wa mazingira kwa kuotesha miti ya Bustani na hata ile ya matunda kwenye eneo Maalum lililotengwa umezingatiwa katika kuona Jiji hilo linakuwa la kupendeza na kufikia hadhi ya kuwa Jiji la Kijani { Green City}.
Mlima uliopo kati kati ya Mji Mpya ndani ya Jiji la Dodoma utawekewa alama Maalum itakayoambatana na Maandishi na Taa wakati wa usiku ukitoa ishara ya kumtambulisha Mtu ye yote anayesafiri kuelewa kwamba anaingia  Ndani ya Mji Mpya wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.