Habari za Punde

Kampuni ya MECCO Yatiliana Saini na Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mwasiliano Zanzibar Ujenzi wa Barabara ya Fuoni Hadi Kibonde Mzungu.

Eneo la barabara ya zamani eneo la Fuoni itakoyoazia barabara hiyo na kuunganishwa katika eneo la daraja jipya la kibondemzungu tayari wananchi wa kando ya barabara hiyo wameaza kuvunja nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara hiyo mpya inayotarajiwa kuaza ujenzi wake hivi karibuni
Na.Mwandishi Wetu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg.Mustafa Aboud Jumbe tarehe 30 Julai, 2019 ametiliana saini Mkataba wa Nyongeza wa Ujenzi wa sehemu ya Barabara kutoka Fuoni Polisi hadi Kibonde Mzungu yenye urefu wa kilomita 1.2 na Kampuni ya Mwananchi Engineering Contracting Company, (Mecco).
Mara baada ya utiaji saini huo Katibu Mustafa ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha ujenzi huo unakwenda vyema na unaenda sambamba na makubaliano yao ili barabara hiyo iwe yenye kiwango na iweze kupitika kwa muda mrefu. 
Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo amesema kutokana na umuhimu wa sehemu hiyo Mkandarasi huyo ataanza kazi tarehe 1 ya mwezi wa 8 na ujenzi huo unatarajiwa kujengwa kwa kipindi cha miezi sita.
Hivyo amewaomba wananchi wa maeneo hayo kutoa mashirikiano ya dhati kwa Mkandarasi ili mradi huo uweze kumalizika kwa wakati bila ya changamoto yoyote. 
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Kampuni ya Mecco Injinia Nassor Ramadhan ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kwa imani kubwa inayoipa kampuni yao kwa kuweza kuwaongeza tena mkataba huo wa nyongeza kwa kipande hicho cha barabara ambapo alisema kwamwe hawatoiangusha Serikali na kuhakikisha wanajenga kwa kiwango cha hali ya juu. 
Aidha, Injinia Nassor amesema kwa vile kampuni yao ndio iliyojenga barabara ya kutoka Mwanakwerekwe hadi Fuoni (Kituo cha Polisi) pamoja na sehemu ya Kibonde Mzungu na ina uzoefu wa kutosha katika masuala hayo watahakikisha barabara hiyo wataikabidhi kazi hiyo kwa muda muafaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.