Habari za Punde

Mkoa wa Kaskazini Unguja unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

Na Mwashungi Tahir    Maelezo  
Taarifa ya utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi imeeleza kuwa Mkoa wa Kaskazini Unguja unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikilinganishwa na Mikoa mingine ya Zanzibar.
Aidha Utafiti huo umeeleza kuwa Wananchi wa Kisiwa cha Pemba wanakabiliwa na tatizo la kufanya mapenzi bila kutumia kinga za maambukizi hayo.
Hayo yameelezwa na Sophy Mohamed kutoka katika Kitengo shirikishi cha Wizara ya Afya wakati akiwasilisha taarifa ya utafiti wa Viashiria na matokeo ya ukimwi wa mwaka 2016-2017 kwa Zanzibar.
Amesema kuna haja kwa wanajamii kubadili mwenendo na tabia kwa kufahamu njia za maambukizi na kuweza kuepukana nazo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mihayo Juma Nhunga wakati akifungua mkutano wa kuwasilisha Taarifa hizo amesema  Serikali imekuwa ikichukua jitihada mbali mbali kwa kushirikina na washirika wa maendeleo na wadau tofauti ili kuyadhibiti maradhi ya ukimwi.
Amesema baada ya kugundulika maradhi hayo tafiti mbali mbali zilifanyika zikiwemo zile ambazo ni mahsusi kwa Zanzibar na zile zinazohusisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kupunguza kasi ya maradhi hayo.
Aidha Nhunga ametoa wito kwa vyombo vya habari kutoa taarifa zenye vyanzo sahihi ili kuepuka kuleta taharuki katika jamii.
Katika Mkutano huo Mada mada mbali mbali pia ziliwasilisha ikiwemo unyanyapaa kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.