Habari za Punde

Tamasha la Utalii Takonga Nyoyo za Wananchi Kisiwani Pemba.

WANANCHI mbali mbali wa Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba wakishudia mtanange wa upigaji dufu, wakati wa tamasha la tatu la utalii na michezo lililofanyika katika kiwanja Cha mpira Wingwi Njuguni
NAIBU Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,  Chumu Kombo Khamis akiwaongoza wananchi mbali mbali waliofurika katika kiwanja Cha Wingwi Njuguni wakati wa Mashindano ya dufu ikiwa ni muendelezo wa tamasha la tatu la utalii na michezo ambalo linaendelea Kisiwani Pemba
WANAFUNZI wa Almadrasatul Jabal Hiraa ya Wete wakionesha uwezo wao wa kucheza dufu wakati wa Mashindano ya dufu ikiwa ni muendelezo wa tamasha la tatu la utalii na michezo ambalo linaendelea Kisiwani Pemba mashindano hayo ambayo yalifanyika katika Viwanja vya Wingwi Njuguni Wilaya ya Micheweni Pemba.
( PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.