Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene (kushoto) akizungumza na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud (katikati)
alipomtembelea Ofisini kwake Vuga kujitambulisha. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mihayo Juma Nunga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud akimuonesha maeneo mbalimbali ya Mji wa Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George
Boniface Simbachawene baada ya kumtembelea na kufanya nae mazungumzo Ofisini
kwake.
Mratibu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Khalid Bakari Hamrani (wa pili kulia) akimpa maelezo Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene
kuhusu ujenzi unaoendelea wa jengo la Kituo cha Afya Kianga Wilaya ya Magharibi
A Mkoani Mjini Magharibi unaojengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
na kusimamiwa na wananchi wenyewe. Kulia ni Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya
Makamu wa Rais Lupi Mwaikambo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene akikagua maendeleo ya ujenzi wa
mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kianga Wilaya ya Magharibi A Mkoani Mjini
Magharibi unaojengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na kusimamiwa
na wananchi wenyewe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene akizungumza alipotembelea eneo la
Kilimani mjini Zanzibar kwenye mradi wa miti ya mikoko kando ya Bahari ya Hindi
ili kuhifadhi mazingira ikiwa ni sehemu ya ziara yake. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Farhat Ali
Mbarouk.
HABARI NA PICHA ZOTE KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
No comments:
Post a Comment