Habari za Punde

Yaliyojiri Ufungaji wa Maonesho ya Kilimo Zanzibar Viwanja Vya Dole Kizimbani Unguja.

 MUHANDISI wa Kampuni ya Davis na Shirtilitt, Partson Mwangomile, akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, namna ya utoaji wa huduma za vifaa vya kusambazia maji, katika maonesho ya nanenane yaliofungwa leo Kizimbani Dole.
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akiangalia bidhaa ya dagaa kavu lililotengenezwa na wajasiria mali kutoka vikundi vya wakulima na wafugaji kutoka Pemba, katika maonesho ya nanenane yaliofungwa leo Kizimbani Dole Wilaya ya Magharibi ‘A’Farida Rajab Taufik, akisoma utenzi wakati wa sherehe za ufungaji wa maonesho ya maadhimisho ya siku ya wakulima nanenane, katika viwanja vya maonesho Kizimbzni Dole Wilaya ya Magharibi ‘A’
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Mariam Juma, akizungumzia mafanikio yaliopatikanwa katika maonesho ya nanenane ya mwaka huu kabla ya kughairishwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi hook Kizimbani Dole.

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akihutubia wakati wa hafla ya ufungaji wa Maonesho ya Kilimo Zanzibar yaliofanyika katika viwanja vya Dole Kizimbani Unguja Wilaya ya Magharibi ‘A’Unguja
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza kwa wajasiria mali kutoka Pemba, Mafunda Bakari Ali, katika maonesho ya nanenane yaliofungwa leo huko Kizimbani Dole Wilaya ya Magharibi ‘A’
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa Mashirika ya Umma, Naibu Mkurugenzi Benkin ya Watu wa Zanzibar PBZ, Khadija Shamte, katika maonesho ya nanenane yaliofungwa leo huko Kizimbani Dole Wilaya ya Magharibi ‘A’
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.