Habari za Punde

Maalim Seif Hana Mamlaka ya Kutumia Mafanikio ya CUF na CCM Kuihusisha na ACT Wazalendo.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CUF Ndg. Abass Juma Muhuzi, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar.
Na.Mwanajuma Juma -Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Ndg.Abbas Juma Muhunzi amesema kuwa Maalim Seif hana mamlaka ya kutumia mafanikio ya CUF na CCM kuihusisha ACT Wazalendo.
Kauli hiyo aliitowa katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa suala la muafaka lilikutanisha vyama viwili ambavyo ni CUF iliyowakilishwa na Maalimu Seif akiwa Katibu Mkuu na CCM iliwakishwa na Dkt. Amani Abeid Karume akiwa Rais wa Zanzibar na wala haukuitwa muafaka wa Maalim Srif na Karume kwa sababu halikuwa suala binafsi hata kama alianzisha yeye.
Hivyo alisema kuwa kitendo chake cha kutumia agenda na mafanikio ya CUF  alichokihama na kukinyang’anya mali zake na hata kukichomea bendera zake ni mwendelezo wa vitendo vya jinai anavyokifanyia   chama cha CUF.
“Na kwa suala la muafaka pia Maalim Seif amekifanyia jinai Chama Cha Mapinduzi”, alisema Muhunzi na kuongeza kuwa mimi sikushangaa niliposikia kongamano lake la maadhimisho ya maridhiyano ya wazanzibari lilizuiwa”.
Sambamba na hilo alisema kuwa washauri wabovu ndio waliomfikisha maalimu Seif pahala pa kushindwa kufikia muafaka na Mwenyekiti wake katika chama alichokianzisha.
Hata hivyo alisema kuwa sio busara vitendo vinavyofanywa na wafuasi wa ACT Wazalendo la kuwatusi viongozi wa CUF na kudahini kwamba hawezi bali wao wanachoamini kuwa sio sera ya chama chao na wanaamini kwamba katika marifhiyano kwa vitendo na pia si utamaduni wao wa kutukanana hadharani.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Chama hicho Mussa Haji Kombo alisema kuwa katika miaka ya nyuma siasa ilikuwa na uwadui mkubwa lakini sasa hivi kupitia maridhiyano hali imekuwa shuwari na wananchi wanaishi kwa amani na utulivu.
Hivyo aliwataka wanachama  wao ambao wamehama na kujiunga na ACT Wazalendo warudi katika CUF kwani kubakia huko ni kujiweka katika mazingira hatarishi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.