Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Kiwanda Cha Cotex Mtaa wac Chumbuni Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua eneo la Kiwanda cha Cotex kilichosita kufanya kazi kwa Miaka kadhaa ambacho tayari ameshajitokeza Muwekezaji anayetaka kukifufuwa upya.
 Baadhi ya mashine zilizochakaa zikiwa ndani ya Majengo ya Kiwanda cha Nguo cha Cotex kilichopo Mtaa wa Chumbuni Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi.
Moja kati ya Magari Matano yakifahari yaliyomo kwenye majengo ya Kiwanda cha Nguo cha Cotex ambayo Wizara ya Biashara imewasiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuyakagua ili kujiridhisha iwapo yapo kihalali.
Balozi Seif  akisisitiza nia ya Serikali ya kutaka Kiwanda cha Cotex kifufuke na kuanza kazi ili kitoe ajira kwa WSananchi na kuongeza Mapato ya  Taifa.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis.OMPR.                                                                                                                     
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshamua kuipa Kampuni ya Uwekezaji ya Basra Textile Milles kufufua upya Kiwanda cha Nguo cha Cotex kilichopo Mtaa wa Chumbuni kwa shughuli za Uwekezaji katika azma yake ya kuimarisha Sekta ya Viwanda Nchini.
Uamuzi huo wa Serikali kuu umekuja kufuatia Kampuni iliyopewa fursa hiyo kushindwa kuitumia vyema nafasi hiyo na hatimae kuamua kuiuza kwa Kampuni nyengine katika kipindi cha zaidi ya Miaka 25 tokea Kiwanda hicho kushindwa uzalishaji kilichokuwa kikitoa ajira kwa Watu kadhaa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alisema hayo wakati alipofanya ziara fupi kuangalia eneo la Kiwanda hicho ambalo limekuwa na magofu ya Mashine bila ya mabadiliko yoyote ya Uwekezaji hali iliyoipelekea Serikali kufanya uamuzi huo.
Balozi Seif alisema zipo taratibu za Uwekezaji zilizowekwa sahihi na Serikali kupitia Taasisi zake ambazo Kampuni au Muwekezaji analazimika kuzifuata, kinyume na utaratibu huo ndipo yanapokuja maamuzi ya Serikali kutengua Mkataba dhidi ya yule aliyeshindwa kufanya hivyo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuagiza Uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar kuhakikisha kwamba zile mali za Muwekezaji aliyeshindwa kukiendeleza Kiwanda hicho zinazondoshwa ili kumpisha Muwekezaji aliyekuwa tayari kufanya kazi hiyo.
Alisema kiwanda hicho ni miongoni mwa maeneo yanayoweza kusaidia nafasi nyingi za ajira wakati kitapofanya kazi jambo ambalo litakwenda sambamba na harakati za Serikali za kuimarisha Viwanda Nchini ili kuongeza mapato na kustawisha maisha ya Wananchi wake.
Mapema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Nd. Ali Khamis Juma alimueleza Balozi Seif  kwamba Muwekezaji huyo alipewa agizo la kuondoka na kuhamisha Mali zake baada ya kushindwa kukiendeleza Kiwanda cha Cotex kwa Miaka mingi sasa.
Nd. Ali alisema Wizara ya Biashara kwa kushirikiana na vyombo vya Dola imelazimika kuchukuwa hatua ya kumuondosha kwa nguvu kutokana na ukaidi wake uliopelekea kufunga makufuli kwenye milango mbali mbali ndani ya Majengo ya Kiwanda hivyo.
Pamoja na mambo mengine Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Biashara na Viwanda alieleza kwamba Wizara hiyo imeshawasiliana na Mamalaka ya Mapato Tanzania {TRA} kufanya ukaguzi wa Magari Matano ya Thamani kubwa yaliyomo ndani ya Kiwanda hicho ambayo hayana nambari za usajili ili Serikali ipate kujiridhisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.