Mtanzania gwiji wa Karate Sensei Rumadha Fundi ametunukiwa shahada ya Dan ya 5 na balaza la Karate la dunia "Okinawa Goju Ryu" katika afla maalumu iliyofanyika mjini Vienna ,Austria mapema wiki hii,ambapo magwiji wa balaza hilo lenye makao yake kule Okinawa ,Japan mara hii waliwaita wataalamu na waalimu wa karate wa kimataifa wanaotambuliwa na baraza hilo katika Semina maalumu na kuwapa mitihani ya kupima viwango vyao ,Tanzania na bara la afrika limewakilishwa na mwalimu mkongwe wa Karate " Goju Ryu" Bw.Sensei Rumadha Fundi mwenye uzoefu wa zaidi ya takribani miaka 38 katika tasinia hiyo na ndiye anayetambuliwa lasmi na baraza hilo la dunia.Sensei Rumadha Fundi mwenye makao yake nchini Marekani pia ni mwalimu nguli Guru wa mitindo ya YOGA. watanzania na wafrika kwa ujumla tuna haki yya kujivunia mtaalamu huyu mwenye rekodi ya kiwango cha kutambuliwa kimataifa na baraza la dunia la Karate.
TANZANIA KUZINGATIA USAWA WA KIJINSIA KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU 2030
-
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Serikali itaendelea kuzingatia ushirikishwaji wa masuala ya kijinsia
kufikia Mpango wa Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 katika ...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment