Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Azungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ikulu Zanzibar, wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza haja kwa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuongeza mashirikiano pamoja na kuutunza na kuuenzi Utawala Bora ili mafanikio zaidi yaweze kupatikana.

Hayo aliyasema leo, Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati ilipowasilisha utekelezaji wa Mpango Kazi wa Julai  2018 hadi Juni 2019 sambambana Mpango Kazi wa mwaka 2019/2020.

Alieleza kuwa Ofisi hiyo inahusika na Utumishi wa Umma na Utawala Bora hivyo, nivyema ikasimamiwa ipasavyo kwa kuuenzi na kuutunza Utawala Bora kwani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio nchi ya mwanzo iliyoanzisha Ofisi ya Utawala Bora kwa kupitia serikali zake zote mbili ikifananishwa na nchi nyingi za barani Afrika.

Hivyo, Rais Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar sio mwanagenzi wa Utawala Bora huku akitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa maadili ni suala muhimu kwa viongozi na kiongozi asiekuwa na maadili hawezi kuongoza.

Rais Dk. Shein alipongeza Ofisi hiyo kwa dhati kutokana na jitihada zao kwa kufanyakazi kwa bidii na kufanya vizuri katika uwasilishaji wao sambambana kufanya jitihada kubwa katika kuwatumikia wananchi wa Zanzibar.

Alieleza kuwa kazi zote zinazofanywa na Mawiziri ni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hivyo, kazi ya kuwahudumia wananchi ni za watu wote na kutumia fursa hiyo kuwaopongeza kwa kufanyakazi kwa mashirikiano kwani hatua hiyo ndio ili yowafikisha hapo.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein alisisitiza haja kwa Ofisi hiyo kuendeleza mashirikiano waliyonayo ili waweze kupata mafanikio zaidi kwani mafanikio waliyopatikana ni ya watu wote na sifa zinazopatikana ni za wananchi wote wa Zanzibar.
Nae Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee aliipongeza kazi nzuri ya uwasilishaji iliyofanywa na Ofisi hiyo huku akisisitiza kuwa katika masuala ya utumishi wa umma Ofisi hiyo iwe mfano sambamba na kujua kuwa wanasimamia utawala wa umma hivyo ni vyema wawe kioo kwa wengine.

Makamo wa Pili wa Rais Zanzibarv Balozi Seif Ali Idd kwa upande wake alitoa pongezi kwa Ofisi hiyo kwa uwasilishaji mzuri wa Mpango Kazi wake na kueleza kuwa Ofisi hiyo ina kazi muhimu hasa katika suala la kupambana na rushwa na uhujumu wa uchumi.

Aidha, alieleza suala zima la maadili kwa viongozi ambalo linasimamiwa na Ofisi hiyo hivyo, alisisitiza haja kulisimamia vyema suala hilo ili kuhakikisha viongozi wanakuwa na maadili mema.

Akisoma muhtasari wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo, Kaimu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe.Khamis Juma Mwalim alieleza vipaumbele vya Ofisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuanza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi. 

Kwa maelezo ya Waziri huyo, vipaumbele vyengine ni kuwezesha shughuli za Serikali na utoaji wa huduma kufanyika kielektroniki, kuendelea kutayarisha miongozo ya Utumishi wa Umma na kusimamia utekelezaji wake, kutekeleza program yamabadilikokatikautumishiwaummanakuimarishausimamiziwamisingiyaUtawala Bora.

Aidha, alielezakuwautekelezajiwavipaumbelehivyoumezingatiaDirayamaendeleoya Zanzibar 2020, IlaniyaUchaguziya CCM kwamwaka 2015/2020, MpangowaKukuzaUchuminaKupunguzaUmasikini Zanzibar (MKUZA III) naMalengoyaMaendeleoEndelevuna Sera zaKisekta.

NaoviongoziwaOfisihiyowalielezakuwautawala bora umeimarikahapanchininakumekuwanaviashiriavinavyooneshautawala bora hasakatikamatumiziyafedhazaSerikalisambambanaushirikishwajimzuriunaofanywahasakwakupitiavikaohivyoalivyovianzishaRais Dk. Sheinnakutumiafursahiyokwakumpongeza.

ViongozihaowalielezakuwaUtawala bora kwaupandewa Zanzibar umepigahatuakubwasanahaliambayoimepelekea Zanzibar kupigahatuakubwakatikasualahilonakusisitizakuongezwakasizaidiiliutawala bora usijekuyumba.

Sambambanahayoviongozihaowaliahidikuendeleakusimamiamisingiyautawala bora sambambanakusimamiamaadilinataratibuzautawala bora.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.